Hizbullah: Saudi Arabia inafanya juhudi za kusaidia Israel iendelee kuwepo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25672-hizbullah_saudi_arabia_inafanya_juhudi_za_kusaidia_israel_iendelee_kuwepo
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hii leo watu wote wameelewa wazi kwamba, Saudi Arabia inafuatilia kuwa na uhusiano na Israel na inafanya juhudi za kuusaidia utawala huo vamizi uendelee kuwepo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 26, 2017 12:47 UTC
  • Hizbullah: Saudi Arabia inafanya juhudi za kusaidia Israel iendelee kuwepo

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hii leo watu wote wameelewa wazi kwamba, Saudi Arabia inafuatilia kuwa na uhusiano na Israel na inafanya juhudi za kuusaidia utawala huo vamizi uendelee kuwepo.

Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon sambamba na kubainisha kwamba, Saudia haiuingi mkono muqawama ameongeza kuwa, utawala wa Aal Saud umetuma nchini Syria makunfdi ya kitakfiri ili kuhudumia fikra za Kizayuni.

Amesema,  mazungumzo ya Astana, Kazakhstan kuhusiana na Syria ni juhudi za kutekeleza usitishaji vita na kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa raia wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Wanamapambano wa Hizbullah

 

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon aidha amesema, mazungumzo hayo kimsingi lengo lake lilikuwa ni kutekelezwa usitishaji vita na kwa kiwango fulani yalikuwa na mafanikio.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria kushindwa mtawalia Saudi Arabia huko nchini Yemen na kubainisha kwamba, ni muhali kwa taifa la Yemen kushindwa katika vita vyao na wavamizi wa Saudia na washirika wake na kwamba Wayemen kamwe hawatauruhusu utawala wa Saudia uchukue hatamu za uongozi na kuamua hatima ya nchi yao.