-
Makumi ya wahajiri wajifungia kwenye kontena Libya
Nov 15, 2018 00:03Makumi ya wahajiri wamejifungia kwenye shehena iliyoko ndani ya meli moja katika mji bandari wa Misrata kwa muda wa siku tano sasa baada ya kuokolewa, wakisisitiza kuwa Libya ni nchi hatari sana kwao.
-
Zaidi ya watu 2000 wamepoteza maisha 2018 wakijaribu kuvuka Mediterania
Nov 07, 2018 13:18Idadi ya watu waliopoteza maisha wakivuka bahari ya Mediteranea mwaka huu wakitafuta hifadhi Ulaya imepindukia 2000 baaada ya maiti 17 kupatikana kwenye ufukwe wa Hispania wiki hii.
-
Trump kuwapa kibali wanajeshi kuwapiga risasi wahamiaji katika mpaka wa Mexico
Nov 02, 2018 03:54Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa, maelfu ya wanajeshi wa nchi hiyo watakaotumwa katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico huenda wakalazimika kuwapiga risasi wahajiri wanaotoka katika nchi za Amerika ya Kati na wanaotaka kuingia Marekani kupitia mpaka huo.
-
Makumi ya wajahiri wahofiwa kufa maji pwani ya Uturuki
Oct 10, 2018 10:49Makumi ya wahajiri wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Uturuki ya Aegean.
-
Wahajiri 34 waaga dunia katika bahari ya Mediterania
Oct 03, 2018 03:51Wahajiri wasiopungua 34 wameaga dunia baada ya boti yao kupata hitilafu magharibi mwa bahari ya Mediterania, huku wengine 26 wakinusurika kifo. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Wahajiri la Umoja wa Mataifa.
-
Wahajiri 466 waokolewa katika Bahari ya Mediterrania
Sep 30, 2018 23:08Idara ya Mabaharia wa Uhispania imetangaza kuwa, wahajiri 466 waliokuwa mbioni kuvuka Bahari ya Mediterrania na kuingia barani Ulaya wameokolewa wakiwa ndani ya boti kumi hafifu katika maji ya Uhispania.
-
Mamia ya wahajiri waokolewa katika maji ya Uhispania
Sep 24, 2018 04:38Jumuiya ya Misaada ya Uokoaji wa Baharini ya Hispania imetangaza kuwa, zaidi ya wahajiri 440 waliokuwa mbioni kuvuka Bahari ya Mediterrania na kuingia barani ulaya wameokolewa majini.
-
Morocco yazuia maelfu ya wahajiri haramu kutumia ardhi ya nchi hiyo
Sep 07, 2018 20:53Viongozi wa Morocco wametangaza kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, serikali ya nchi hiyo imefanikiwa kuzuia wahajiri haramu 54 elfu kutumia ardhi ya nchi hiyo kuelekea barani Ulaya.
-
Italia yakata misaada yake kwa Umoja wa Ulaya (EU)
Aug 26, 2018 02:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia ametangaza kuwa nchi hiyo imekata misaada yake kwa Umoja wa Ulaya kufuatia kuendelea mivutano kati ya umoja huo na Italia kuhusu suala la wahajiri waliokwama katika meli ya gadi ya pwani ya Italia kwa jina la Diciotti (Dichuti).
-
Umoja wa Mataifa wataka kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa wahajiri barani Ulaya
Aug 25, 2018 09:20Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kutekeleza majukumu yao kuhusiana na wahajiri 150 wanaotangatanga katika meli ya Gadi ya Pwani ya Italia.