-
Makumi ya watu wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Ethiopia
Dec 15, 2018 07:18Watu wasiopungua 21 wameuawa katika mapigano ya kikabila kusini mwa Ethiopia.
-
Umoja wa Mataifa: Wanahabari 88 wameuawa mwaka huu 2018
Nov 02, 2018 07:32Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema jumla ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine katika sekta ya upashanaji habari 85 wameuawa tokea mwanzoni mwa mwaka huu 2018 hadi sasa katika sehemu mbalimbali duniani.
-
Jeshi la Israel laendeleza ukatili wake, laua Wapalestina 5 Ghaza
Oct 27, 2018 05:52Kwa akali Wapalestina watano wameuawa shahidi huku mamia ya wengine wakijeruhiwa baada ya jeshi la Israel kuwamiminia risasi na kuvurumishia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Idadi ya vifo katika miripuko wa Somalia yaongezeka
Oct 15, 2018 07:51Idadi ya wahanga wa mashambulio mawili ya kujiripua kwa mabomu iliyotokea kusini magharibi mwa Somalia imeongezeka. Taarifa zinasema kuwa watu 20 wamepoteza maisha na wengine 40 wamejeruhiwa katika miripuko hiyo miwili iliyopishana kwa dakika chache tu.
-
Saudi Arabia yaua raia 79 Yemen masaa 48 yaliyopita
Oct 10, 2018 08:04Duru za usalama na hospitali nchini Yemen zimeripoti kuwa ndege za kivita za Saudi Arabia zimeua raia wasiopungua 79 katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita katika mkoa wa al Hudaydah pekee.
-
Watu 50 wafa, 100 wachomwa na moto wa lori la mafuta DRC
Oct 06, 2018 15:29Watu wasiopungua 50 wamepoteza maisha na wengine 100 wamepata majeraha ya moto baada ya lori la mafuta lililopinduka kuanza kuwaka moto huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Watu 16 wauawa katika shambulio la waasi mashariki mwa DRC
Sep 23, 2018 16:00Watu 16 wameuawa katika shambulio jipya la waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Mapigano yashtadi Libya, waliouawa Tripoli wapindukia 96
Sep 21, 2018 13:52Wizara ya Afya nchini Libya imetoa indhari juu ya kushadidi mapigano katika mji mkuu Tripoli, ambapo idadi ya waliouawa katika ghasia hizo imeongezeka na kufikia watu 96, wakiwemo raia.
-
Watu 19 wauawa katika shambulio la wanamgambo kaskazini mashariki mwa Nigeria
Aug 20, 2018 07:49Duru za habari zimeripoti kuwa watu 19 wameuliwa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo katika kijiji kimoja kilichoko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Wahajiri wanne wapoteza maisha baada ya boti kuwaka moto Tunisia
Aug 19, 2018 15:18Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imetangaza habari ya kupoteza maisha wahajiri wanne baada ya boti yao kuungua moto katika fukwe za Sfax, mashariki mwa nchi hiyo.