Dec 26, 2018 07:24 UTC
  • Wanajeshi 14 wauawa katika shambulio la Boko Haram nchini Nigera

Wanajeshi wasiopungua 14 wameuawa nchini Nigeria wameuawa kufuatia shambulio la kkundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Yobe kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema kuwa, wanajeshi hao wameuawa baada ya kundi la Boko Haram kufanya shambulio la kushtukiza dhidi ya msafara wa wanajeshi na polisi uliokuwa njiani kwenda kuutekeleza majukumu yake.

Jeshi la Nigeria aidha limesema kuwa, limeanzisha operesheni kali katika jimbo la Yobe la kuwasaka wananchama hao wa Boko Haramu waliofanya shambulio dhidi ya wanajeshi.

Kanali Onyema Nwachukwu msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, shambulio hilo lilitokea nje kidogo ya mji wa Damaturu ulioko katika jimbo la Yobe.

Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianza kufanya mashambulizi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2009 na tangu wakati huo hadi hivi sasa limeshasababisha zaidi ya watu 20 elfu kuuawa na zaidi ya milioni mbili na laki sita wengine kuwa wakimbizi.

Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria

Kundi hilo Haram limetangaza utiifu wake kwa genge la kigaidi la Daesh na limekuwa likifanya mashambulizi katika nchi nne zinazopakana na Ziwa Chad za Nigeria, Chad, Niger na Cameroon.

Nchi hizo nne zimeunda kikosi cha pamoja cha kupambana na magaidi wa Boko Haram lingawa hadi hivi sasa zimeshindwa kuliangamiza genge hilo la wakufurishaji. Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria ameendelea kukosolewa kutokana na kushindwa kutekkeleza ahadi yake ya kuliangamiza kundi hilo la kigaidi.

Tags