Mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo mjini Tehran
(last modified Thu, 15 Dec 2016 05:29:12 GMT )
Dec 15, 2016 05:29 UTC
  • Mkutano wa kimataifa wa  Umoja wa Kiislamu umeanza leo mjini Tehran

Duru ya 31 ya mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na shakhsia, wanazuoni na wanafikra kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mkutano huo utakaofanyika kwa muda wa siku tatu unabeba anuani isemayo: "Umoja na Udharura wa Kupambana na Harakati ya Utakfiri" unahudhuriwa na wanafikra kutoka zaidi ya nchi 50 duniani zikiwemo, Malaysia, Russia, Indonesia, Iraq, Lebanon, Thailand, Algeria, Uingereza, Marekani, Australia, Tunisia, China, Misri, Kenya na Tanzania.

Washiriki wa kigeni wa mkutano huo jana walizuru haram ya Imam Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutoa heshima zao.

Mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu hufanyika kila mwaka mjini Tehran kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Wiki ya Umoja wa Kiislamu.