UN ina wasiwasi kuhusu kukandamizwa waandamanaji wa Kiafrika huko Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i101880-un_ina_wasiwasi_kuhusu_kukandamizwa_waandamanaji_wa_kiafrika_huko_israel
Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyowatendea waandamanaji wa Kiafrika katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 05, 2023 04:07 UTC
  • UN ina wasiwasi kuhusu kukandamizwa waandamanaji wa Kiafrika huko Israel

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyowatendea waandamanaji wa Kiafrika katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Ghasia na maandamano makubwa yalitokea Jumamosi mjini Tel Aviv yakishirikisha wazayuni wenye asili ya Eritrea na Sudan waliohamishiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

Ghasia hizo zilizokuwa na umwagaji damu, zilitokea kati ya vikosi vya polisi vya utawala dhalimu wa Israel na wahamiaji wenye asili ya Afrika, haswa Waeritrea na Wasudan, ambapo karibu watu 200 walijeruhiwa.

Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, ameelezea wasiwasi wake kuhusu ukatili mkubwa wa polisi wa Israel dhidi ya waandamanaji wa Kiafrika na kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Nimeshtushwa na idadi kubwa ya waliojeruhiwa katika maandamano ya watu wenye asili ya Eritrea" huko Israel.

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusiana na ukatili huo. 

Volker Türk pia amesisitiza ulazima wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuepuka kueneza chuki.

Televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeripoti kwamba, idadi ya waliojeruhiwa katika machafuko hayo ya Wazayuni wenye asili ya Kiafrika na askari wa Israel huko Tel Aviv imefikia watu 170, na kwamba 20 kati yao wako katika hali mbaya.

Ushahidi unaonyesho kuwa, kuna agizo la dharura la baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu la kuwatimua Mayahudi wenye asili ya Afrika ambao walishiriki katika ghasi za Jumamosi, na jambo hili inaonyesha kwamba, serikali ya kibaguzi iliyoko madarakani Tel Aviv ilikuwa inasubiri fursa ya kuchukua hatua dhidi ya watu hao wenye asili ya Afrika.