Ansarullah: Ukaliaji mabavu wa Marekani hautadumu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i102638-ansarullah_ukaliaji_mabavu_wa_marekani_hautadumu
Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametaja uwepo wa vikosi vamizi vya nchi za Magharibi na Marekani huko Yemen kuwa ni ukaliaji mabavu na akasema, takwa la wananchi wote wa Yemen ni kuondoka kwa vikosi hivyo vamizi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 25, 2023 01:20 UTC
  • Ansarullah: Ukaliaji mabavu wa Marekani hautadumu

Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametaja uwepo wa vikosi vamizi vya nchi za Magharibi na Marekani huko Yemen kuwa ni ukaliaji mabavu na akasema, takwa la wananchi wote wa Yemen ni kuondoka kwa vikosi hivyo vamizi.

Baadhi ya duru za habari za Yemen hivi karibuni ziliripoti kuwa wanajeshi kadhaa wa Marekani wamewasili katika maeneo ya mashariki mwa Yemen. Katika upande mwingine, duru za kuaminika zimetangaza kuwa, wanajeshi vamizi wa Uingereza wanataka  kuanzisha kambi ya kijeshi katika mkoa wa Hadhramaut mashariki mwa Yemen. 

Vikosi vamizi vya Marekani mashariki mwa Yemen 

Ali al Qhoom Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah amesema kuwa serikali ya Sana'a inafuatilia kwa karibu uwepo moja kwa moja wa Marekani na Magharibi huko Yemen; hatua inayohesabiwa kuwa ukiukaji wa kanuni na sheria zote za kimataifa. 

Al Qhoom amesisitiza kuwa Ansarullah haitafumbia macho uwepo wa nchi hizo vamizi kwa kuzingatia uwezo wa sekta yake ya kijeshi. 

Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameongeza kusema kuwa Watu wa Yemen hawakubali uwepo wa Marekani na wale wote wanaohatarisha usalama, utulivu, mamlaka na umoja wa ardhi ya nchi hiyo.