HAMAS yaishukuru Iran kwa inavyoipa uzito na umuhimu kadhia ya Palestina
Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa inavyoishughulikia na kuipa umuhimu kadhia ya Palestina.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Khalil Al-Hayah, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amesema, wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian na kufanya mashauriano naye juu ya kuunda mhimili mkubwa na mpana zaidi ili kukomesha jinai za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel; na kwamba kulingana na suhula zilizonazo, vipi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na serikali za Kiarabu zinaweza kusaidia kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.
Al-Hayah amesisitiza kwa kusema, "tunatumai kuwa nchi zote zitalisaidia taifa la Palestina kufikia lengo na piganio lake tukufu la kuikomboa ardhi hii kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni, kuuangamiza utawala huu ghasibu na kuunda nchi ya Palestina ambayo mji mkuu wake ni Baitul Muqaddas (Jerusalem)'.
Katika mwendelezo wa mashauriano juu ya matukio ya Palestina, jana Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian alikutana na kufanya mazungumzo na Ismail Haniyah, Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na Khalil al-HAyah mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo, mjini Doha, Qatar
Katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, vikosi vya muqawama vya Palestina siku ya Jumamosi ya tarehe 7 Oktoba, vilianzisha operesheni kubwa na ya kipekee iitwayo Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya ngome za utawala khabithi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Kutokana na kushindwa vibaya sana kwa kuangamizwa na kujeruhiwa Wazayuni zaidi ya elfu tano na kutekwa kwa muda baadhi ya vitongoji vya walowezi na vituo vya kijeshi, viongozi wa utawala huo ghasibu wameamuru kufanywa mashambulio ya kinyama ya mtawalia yanayowalenga Wapalestina wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza na kutenda jinai chungu nzima za kivita katika eneo hilo lililowekewa mzingiro.../