Israel: Kukomboa mateka na kulinda roho za raia si kipaumbele chetu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103706-israel_kukomboa_mateka_na_kulinda_roho_za_raia_si_kipaumbele_chetu
Waziri mmoja wa serikali yenye misimamo mikali ya Kizayuni amejigamba kuwa, suala la kukomboa mateka wa Israel na kulindwa roho za raia huko Ghaza, si kipaumbele kwa utawala wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 20, 2023 03:20 UTC
  • Israel: Kukomboa mateka na kulinda roho za raia si kipaumbele chetu

Waziri mmoja wa serikali yenye misimamo mikali ya Kizayuni amejigamba kuwa, suala la kukomboa mateka wa Israel na kulindwa roho za raia huko Ghaza, si kipaumbele kwa utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la FARS limemnukuu waziri huyo wa serikali ya Israel yenye misimamo ya kuchupa mipaka akisema hayo bila ya kisisi na kuongeza kuwa, kulindwa roho za watu au kukombolewa mateka wa utawala wa Kizayuni walioko mikononi mwa wanamapambano wa Palestina si muhimu katika uvamizi wa nchi kavu ambao amedai umepangwa kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza. 

Waziri huyo Mzayuni, Nir Barkat, amesema hayo wakati alipohojiwa na televisheni ya ABC ya Marekani na kuongeza kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni limeshapewa idhini ya kuanzisha vita vya nchi kavu dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kwamba kukombolewa mateka Wazayuni na kuchunga roho za raia si muhimu kwa Israel katika operesheni zake dhidi ya HAMAS hata kama vita hivyo vitadumu kwa muda wa mwaka mzima.

Majigambo hayo ya waziri wa serikali yenye misimamo mikali ya utawala wa Kizayuni yametolewa katika hali ambayo uzoefu wa huko nyuma unaonesha jinsi wanajeshi wa Israel walivyopata vipigo vikali walipojaribu kuanzisha vita vya nchi kavu ndani ya Ukanda wa Ghaza. 

Wanamapambano wa Palestina nao muda wote wamekuwa wakitangaza kwamba wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na wanajeshi wa Israel iwapo watajipa uthubutu wa kijinga wa kuanzisha vita vya nchi kavu dhidi ya Ghaza na kuwakumbusha Wazayuni hao vipigo walivyopata huko nyuma katika mapambano ya mahandaki. 

Licha ya Israel kufanya mashambulio makubwa ya kinyama ya anga, lakini hadi hivi sasa inaogopa kuanzisha vita vya nchi kavu huko Ghaza.