Israel sasa yashambulia makanisa baada ya kushambulia Misikiti na hospitali Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103710-israel_sasa_yashambulia_makanisa_baada_ya_kushambulia_misikiti_na_hospitali_ghaza
Baada ya utawala katili wa Israel kushambulia Misikiti na hospitali za Ukanda wa Ghaza, sasa umeyaelekea makanisa ya ukanda huo na kuua na kujeruhi Wakristo wengi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 20, 2023 03:24 UTC
  • Israel sasa yashambulia makanisa baada ya kushambulia Misikiti na hospitali Ghaza

Baada ya utawala katili wa Israel kushambulia Misikiti na hospitali za Ukanda wa Ghaza, sasa umeyaelekea makanisa ya ukanda huo na kuua na kujeruhi Wakristo wengi.

Kituo cha upashaji habari cha Palestina kimewanukuu watu walioshuhudia wakisema kuwa, jeshi la Israel limeshambulia jengo la Kanisa la Orthodox mjini Ghaza na kuua Wakristo wengi na kujeruhi zaidi ya raia 200 wengine. 

Mlinzi wa kanisa hilo ameiambia televisheni ya al Aqsa kwamba, zaidi ya Wakristo na Waislamu 400 walikuwa wamekimbilia kwenye kanisa hilo kujikinga na mashambulio ya kikatili ya Israel lakini hawakusalimika. 

Kijana mmoja Mkristo wa Ghaza amesikikika akipiga mayowe kwa kite na majonzi makubwa akisema: Wametushambulia! Hakuna sehemu yoyote ya kukimbilia na kubaki salama ndani ya Ghaza! 

Utawala wa Kizayuni wa Israel unatenda jinai kiasi kwamba hata maeneo ya ibada yakiwemo makanisa hayabaki salama

 

Kijana huyo Mkristo ambaye amenusurika kifo baada ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kulishambulia kanisa hilo amesema, wanajeshi wa Israel hawajali raia, wala watoto wadogo, wala wanawake na wala maeneo ya ibada hata ya Wakristo. 

Hivi karibuni mamia ya Wakristo wanaoishi Ukanda wa Ghaza wamekuwa wahanga wa mashambulizi makali ya kikatili yanayofanwa na utawala wa Kizayuni ambao umetangaza wazi kuwa roho za raia si kipaumbele chake katika vita na Wapalestina.

Akihojiwa na televisheni ya ABC ya Marekani, Waziri Mzayuni, Nir Barkat, amesema kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni limeshapewa idhini ya kuanzisha vita vya nchi kavu dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kwamba kukombolewa mateka Wazayuni na kuchunga roho za raia si muhimu kwa Israel.

Kanisa hilo lililoshambuliwa usiku wa kuamkia leo na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza lina historia ndefu na ni kanisa la tatu kwa ukongwe duniani.