WFP yaonya kuhusu tishio kwa maisha ya watu wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103928-wfp_yaonya_kuhusu_tishio_kwa_maisha_ya_watu_wa_gaza
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limeonya kuhusu tishio linalokabili maisha ya watu wa Gaza.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Oct 25, 2023 11:41 UTC
  • WFP yaonya kuhusu tishio kwa maisha ya watu wa Gaza

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limeonya kuhusu tishio linalokabili maisha ya watu wa Gaza.

Kwa mujibu wa CBC, Abeer Etefa, afisa mkuu wa mawasiliano wa WFP nchini Misri, amesema: "Kuna familia ambazo haziwezi kufikiwa na pengine zinakufa kwa njaa."

Afisa huyo wa WFP ameongea kuwa: "Kwa sababu ya kuharibiwa miundombinu na ukosefu wa mafuta, hakuna uwekano wa kusafirisha bidhaa za misaaada ya kibinadamu na malori hayaruhusiwi kusafiri kuelekea Gaza."

Abeer Etefa amesema kuwa, misaada ya kibinadamu inayoruhusiwa kuingia Gaza ni kama "tone kwenye bahari" ikilinganishwa na hali mbaya ya raia katika eneo hili lililozingirwa.

Pia jana, Brian Lander, naibu afisa wa masuala ya dharura wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, alionya kwamba "Gaza inageuka kuwa maafa makubwa ya binadamu."

Afisa huyu wa Umoja wa Mataifa anasema: Baadhi ya watu huko Gaza wanalazimika kuchemsha na kutumia maji ya bahari ili waweze kubakia hai. Ameonya kuwa hali inazidi kuwa mbaya.

Wakati huo huo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imeonya kwamba, unga wa ngano katika Ukanda wa Gaza utaisha katika muda wa chini ya wiki moja.

Ashraf al-Qadara, msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, amesema mapema leo kwamba hawawezi tena kutoa huduma yoyote katika hospitali za Ukanda wa Gaza, na kwamba mfumo wa afya wa eneo hilo linalozingirwa na Israel unaporomoka kikamilifu.