Ansarullah: Adui Mzayuni anafanya jinai mbele ya macho ya walimwengu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103982-ansarullah_adui_mzayuni_anafanya_jinai_mbele_ya_macho_ya_walimwengu
Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen akizungumzia mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina amesisitiza kuwa, adui Mzayuni anafanya jinai mbele ya macho ya walimwengu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 26, 2023 23:02 UTC
  • Ansarullah: Adui Mzayuni anafanya jinai mbele ya macho ya walimwengu

Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen akizungumzia mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina amesisitiza kuwa, adui Mzayuni anafanya jinai mbele ya macho ya walimwengu.

Mohammed Abdul Salam, msemaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, amezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza kuwa ni unyama na ukatili mkubwa.

Abdul Salam ameongeza kusema kuwa, adui Mzayuni anafanya jinai za kinyama mbele ya macho ya walimwengu na kwa himaya na uungaji mkono wa wazi wa Marekani na madola ya Magharibi.

Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa Al-Mayadeen, Abdul Salam ameeleza kuwa, kuwalenga waandishi wa habari wa Gaza na kusini mwa Lebanon na familia zao ni jaribio lililofeli la utawala wa Kizayuni wa Israel la kuzusha hofu na kuwaadhibu kwa kusambaza picha halisi za adui.

 

Ofisi ya Habari ya serikali huko Gaza Palestina imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu utawala haramu wa Israel ulipoanza kufanya mashambulio ya anga katika Ukanda wa Gaza imepindukia 7000 huku makumi ya maelfu ya wengine wakiwa wamejeruhiwa au kutoweka.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, wengi wa mashahidi hao ni wanawake na watoto huku hali ya kibidamu katika Ukanda wa Gaza ikielezwa kuwa inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Tangu kuanza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa siku 16 zilizopita sawa na Oktoba 7, kushambuliwa maeneo ya makazi na umma kwa upande mmoja na kukatwa maji, umeme na uhaba mkubwa wa chakula na dawa kwa upande mwingine, kumewafanya wakazi wa Ukanda wa Gaza kukabiliwa na hali ngumu sana na kupelekea taasisi za haki za binadamu kutangaza hali ya kibinadamu katika eneo hilo kuwa mbaya na ya kutisha.