Mkuu wa Intelijinsia wa jeshi la Kizayuni: Tumeshindwa
(last modified 2023-11-02T02:31:32+00:00 )
Nov 02, 2023 02:31 UTC
  • Mkuu wa Intelijinsia wa jeshi la Kizayuni: Tumeshindwa

Kufuatia utawala wa Kizayuni kukiri kushindwa mbele ya wanamapambano wa Palestina, Mkuu wa Idara ya Ujasusi katika jeshi la utawala huo ghasibu pia amesisitiza akisema:" Sisi tumeshindwa."

Televisheni ya Al Mayadeen jana Jumatano ilitangaza kuwa, Mkuu wa Idara ya Ujasusi katika jeshi la utawala wa Kizayuni (Aman) amekiri kuhusu kushindwa kiitelijinsia na pakubwa utawala huo mkabala wa oparesheni ya "Kimbunga cha Al Aqsa" na kusema: Taasisi ya Aman anayoingoza imefeli; na anabeba dhima kamili ya kufeli kwao mbele ya muqawama wa Palestina.  

Katika upande mwingine, mmoja wa ndugu wa askari wa utawala wa Kizayuni waliouawa katika Ukanda wa Ghaza amesema leo katika mahojiano na vyombo vya habari vya Kizayuni kwamba: Netanyahu (Waziri Mkuu) anapaswa kujiuzulu. Hadi sasa baadhi ya viongozi kadhaa wa kisiasa na kijeshi wa utawala wa Kizayuni wamekiri kushindwa  kwa upande wa kiitelijinsia na kiusalama; na kushindwa taasisi za utawala huo kutabiri uwezekano wa kutekelezwa operesheni ya muqawama wa Palestina ya Kimbunga cha Al-Aqsa. 

Hivi karibuni Netanyahu alijaribu kuvibebesha mzigo wa lawama vyombo vya usalama na kijeshi na kujiondoa hatiani kufuatia kushindwa utawala wa Kizayuni mkabala wa Kimbunga cha Al Aqsa, hata hivyo alikabiliwa na jibu kali kutoka kwa duru za kisiasa, kijeshi na kiusalama za utawala huo na kulazimika kuomba radhi. Hali hii imezua mgogoro mkubwa miongoni mwa viongozi wa kijeshi, kisiasa na kiusalama wa utawala huo ghasibu.

Tags