Jinai zai Israel zaendelea; Wapalestina wengine 19 wauawa Jabaliya
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104246-jinai_zai_israel_zaendelea_wapalestina_wengine_19_wauawa_jabaliya
Wapalestina wengiine 19 wameuawa shahidi kufuatia mashambulio ya anga ya utawala haramu wa Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-05-19T09:45:50+00:00 )
Nov 02, 2023 04:04 UTC
  • Jinai zai Israel zaendelea; Wapalestina wengine 19 wauawa Jabaliya

Wapalestina wengiine 19 wameuawa shahidi kufuatia mashambulio ya anga ya utawala haramu wa Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Mashambulio hayo ya kinyama ya jana usiku yamelenga maeneo kadhaa pia magharibi mwa Gaza na vilevile huko Bait Lahya, al-Karamah na maeneo ya jirani na hospitali ya Kiindonesia na al-Shafa katika Ukanda wa Gaza.

Shambulio hilo linajiri siku moja tu baada ya Wapalestina wasiopungua 400, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, kuthibitishwa kuuawa na kujeruhiwa baada ya mashambulizi ya anga ya utawala katili wa Israel dhidi ya wakimbizi ya Jabaliya katika Ukanda wa Gaza.

Mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala haramu wa Israel huko Gaza tokea Oktoba 7 yamesababisha vifo vya Wapalestina karibu 9,000 na wengine zaidi ya 23,200 kujeruhiwa. Aghalabu ya waliouawa katika hujuma hiyo ya Israel ni wanawake na watoto.

 

Wakati huo huo, habari kutoka Gaza zinasema kuwa, tangu kuanza mashambulio hayo ya kijinai ya utawala katili wa Israel zaidi ya wanafunzi 2500 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa.

Hujuma hiyo ya kinyama inaendeea licha ya miito ya walimwengu ya kusitishwa unyama huo na kuruhusu kupelekwa misaada ya kibinadamu huko Gaza.

Asasi na jumuiya mbalimbali zimeendelea kuonya kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza na kutaka kusitishwa mapigano.