Indhari ya kushtua ya WFP kuhusu watoto Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104402-indhari_ya_kushtua_ya_wfp_kuhusu_watoto_ukanda_wa_gaza
Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ametahadharisha kuhusu hali mbaya inayowakabili watoto wa Kipalestina huko Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Nov 05, 2023 23:29 UTC
  • Indhari ya kushtua ya WFP kuhusu watoto Ukanda wa Gaza

Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ametahadharisha kuhusu hali mbaya inayowakabili watoto wa Kipalestina huko Ukanda wa Gaza.

Cindy H. McCain Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ametoa matamshi ya kushtua kwamba: Akina baba huko Gaza hawajui kama wanaweza kuwalisha watoto wao leo au kama watoto hao watasalia hai hadi kesho. 

McCain amesisitiza kuwa Mpango wa Chakula Duniani unataka kutumwa haraka na salama salimini misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. Kuhusiana na suala hili, Shirika la Afya Duniani (WHO) pia limetangaza katika ripoti yake kuwa: Wamesajili zaidi ya mashambulizi mia moja kwenye vituo vya matibabu huko Gaza tangu tarehe 7 Oktoba iliyopita.  

Jinai za Israel dhidi ya magari ya kubebea wagonjwa na hospitali Ukanda wa Gaza 

Ripoti ya WHO imeongeza kuwa, idadi ya mashahidi huko Gaza tangu kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni Oktoba 7 mwaka huu imefika karibu elfu 10; ambapo kati ya idadi hii tajwa watoto ni karibu elfu nne na wanawake 2,510.  Wakati huo huo ripoti zinasema kuwa watu zaidi ya elfu mbili hawajulikani walipo hadi sasa; ambapo kati ya idadi hiyo watoto ni 1,200 ambao wapo chini ya vifusi.