Utawala wa Kizayuni unatumia mamluki wa Ulaya katika vita vya Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104414-utawala_wa_kizayuni_unatumia_mamluki_wa_ulaya_katika_vita_vya_ghaza
Chombo kimoja cha habari nchini Uhispania kimefichua kuwa, utawala wa Kizayuni unatumia mamluki wa Ulaya katika vita vya Ghaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 06, 2023 03:07 UTC
  • Utawala wa Kizayuni unatumia mamluki wa Ulaya katika vita vya Ghaza

Chombo kimoja cha habari nchini Uhispania kimefichua kuwa, utawala wa Kizayuni unatumia mamluki wa Ulaya katika vita vya Ghaza.

Uungaji mkono wa Wamagharibi kwa utawala wa Kizayuni kwa kisingizio cha kujilinda utawala huo, kivitendo ni ishara ya rangi ya kijani na leseni kwa utawala huo kuendeleza mauaji ya kimbari na kikatili dhidi ya watoto na wanawake wa Kipalestina.

Gazeti la Uhispania la El Mundo limefichua katika mahojiano na Mhispania anayeitwa Pedro Diaz Flores kwamba aliajiriwa katika jeshi la Kizayuni kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Flores amekiri kwa kusema: Niko tayari  kwa ajili ya  pesa, wanalipa vizuri, wanatoa vifaa vizuri, kazi ni ya utulivu, na mshahara wa wiki ni euro 3,900.

Mamluki wa Ulaya

Mhispania huyo amesema, kuhusiana na aina ya kazi yake,  kuwa watu kama yeye hutoa tu msaada wa usalama kwa misafara ya kijeshi ya Israel.

Tarehe 7 Oktoba, wanamuqawama wa Palestina walifanya operesheni ya kushtukiza ya Kimbuga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Ghaza kusini mwa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Tel Aviv. Ili kulipiza kisasi na kufidia kushindwa kwake na kuficha fedhehe hiyo, utawala wa Kizayuni ulifunga vivuko vyote vya Ukanda wa Ghaza na kulishambulia vikali kwa mabomu, na hadi sasa bado unaendeleza mauaji ya kijinai na kimbari dhidi ya watu wa ukanda huo.