Kufichuliwa kuangamizwa Wazayuni tarehe 7 Oktoba na helikopta ya Israel!
Gazeti la Haaretz limeripoti kuwa kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na polisi ya utawala ghasibu wa Israel, helikopta ya jeshi la utawala huo iliwafyatulia risasi Wazayuni waliokuwa kwenye tamasha la muziki jangwani tarehe 7 Oktoba.
Licha ya juhudi za utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wa Magharibi za kupotosha ukweli wa mambo na kuonyesha sura mbaya ya makundi ya muqawama wa Palestina na kuituhumu Hamas kuwa ndiyo iliyohusika na mauaji ya walowezi wa Kizayuni katika operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, lakini uwongo wa wavamizi hao unazidi kudhihirika kila kukicha.
Gazeti la Haaretz la Jumapili asubuhi limeripoti kwamba kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na polisi ya Israel, helikopta ya jeshi iliwafyatulia risasi na kuwaua Wazayuni waliokuwepo kwenye tamasha la muziki wa jangwani tarehe 7 Oktoba.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wapiganaji wa Hamas walioshambulia maeneo ya jeshi la Kizayuni tarehe 7 Oktoba wakati wa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, hata huwakuwa na habari kuhusu kuwepo tamasha la jangwani karibu na mji wa Raim.