Bunge la Bahrain launga mkono kundi la kigaidi la Munafiqin
Wabunge wa Bahrain wametangaza uungaji mkono wao kwa kundi la kigaidi la Munafiqin ikiwa ni katika kuendelezwa siasa za nchi hiyo dhidi ya Iran.
Wawakilishi wengi wa Bunge la Bahrain wametoa taarifa wakiliunga mkono kundi la kigaidi la Munafiqin ambalo limetenda jinai chungu nzima dhidi ya wananchi wa Iran na wa Iraq.
Katika hali ambayo kundi hilo limetekeleza mauaji ya umati dhidi ya maelfu ya wananchi wa Iran na Iraq; wabunge wa Bahrain wamedai kuwa kundi hilo linaheshimika mbele ya wananchi.
Madai hayo yametolewa na wabunge wa Bahrain katika hali ambayo Wabahraini zaidi ya 150 wameuawa, mamia ya wengine kujeruhiwa na wafungwa wa kisiasa elfu tatu wakiwa katika jela za nchi hiyo kufuatia ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Bahrain katika kipindi cha miaka mitano ya kujiri harakati za amani za ukombozi za wananchi wa Bahrain. Licha ya Washia kuunda idadi kubwa ya raia wa Bahrain lakini utawala wa Aal Khalifa umedhamiria kubadili muundo huo wa kijamii kwa kuwaingiza nchini raia wa nchi ajinabi na kisha kuwapatia uraia wa nchi hiyo.