Jeshi la Syria latangaza usitishwaji Vita Idul Fitr
Jeshi la Syria limetangaza usitishwaji vita wa masaa 72 kote katika nchi hiyo kwa munasaba wa Siku Kuu ya Idul Fitr.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Syria SANA, Kamandi Kuu ya Jeshi imetangaza Jumatano kuwa, usitishwaji vita huo umenaza kutekeleza Julai sita hadi saa sita usiku Julai 8.
Wakati huo huo , Rais Bashar al Assad wa Syria alishiriki katika Sala ya Idul Fitr iliyosaliwa katika Msikiti wa Al-Safaa katika mtaa wa Akrama mjini Homs magharibi mwa Syria.
Televisheni ya Syria imemuoneysha Rais Assad akiswali katika safu moja pamoja na Waziri wa Masuala ya Kiislamu Mohammad Abdel-Sattar Sayyed na Mufti Mkuu wa Syria Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun.
Eneo kubwa la Homs lilikuwa limetekwa na magaidi wanaopata himaya ya kigeni lakini kutoka mwezi Mei mwaka 2014 magaidi wamepata piga na ngome yao iko katika eneo moja tu.
Syria ilitumbukia katika vita mwezi Machi 2011 ambapo Umoja wa Matiafa unasema hadi sasa 400,000 wameshauawa huku mamilioni ya wengine wakilazimikwa kuwa wakimbizi. Serikali ya Syria inalaumu baadhi ya nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifakie wake katika eneo yaani Utawala wa Israel, Uturuki, Qatar na Saudi Arabia kuwa ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi wakufurishaji nchini humo.