Wanamuqawama wa Palestina watoa kipigo kikali kwa wanajeshi wa Kizayuni huko Rafah
Wanamapambano wa Palestina wametoa kipigo kikali kwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika mapigano makali yaliyojiri katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, mapigano makali yamejiri kati ya wanamuqawama wa Palestina na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika maeneo ya Tal al Sultan, Tal al Zorab na katika kitongoji cha Al Saud na huko Barksat magharibi mwa mji wa Rafah.
Ripoti ya IRNA imeongeza kuwa, wanamapambano wa Palestina wametoa pigo kubwa kwa wanajeshi ghasibu wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza na kuwaangamiza wanajeshi kadhaa wa utawala huo haramu.
Wakati tunapokea taarifa hii wanajeshi wa jeshi la Israel walikuwa wamefanya shambulio katika nyumba moja katika kambi ya al Jadid huko kaskazini mwa kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nuseirat katikati mwa Gaza.
Wakati huo huo jeshi la Israel limeshambulia eneo la kaskazini mashariki mwa kambi ya al Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.