CNN: Jeshi la Israel linawatumia raia kama ngao za binadamu
(last modified Sun, 27 Oct 2024 07:54:22 GMT )
Oct 27, 2024 07:54 UTC
  • CNN: Jeshi la Israel linawatumia raia kama ngao za binadamu

Televisheni ya CNN ya Marekani imesema katika mahojiano na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni na raia kadhaa wa Palestina na kufichua kuhusu kutumiwa kwa makusudi raia wa Kipalestina kama ngao ya binadamu.

Mtandao wa Sahab umelinukuu shirika la habari lla ISNA na kuripoti kuwa, televisheni ya CNN imeripoti kuwa, jeshi la Israel linawaaamuru raia wa Kipalestina kusalia majumbani mwao, kuelekea mahandakini au katika maeneo yaliyozingirwa wakiwatangaliza mbele kama ngao ya binadamu kuzuia hatari ambayo ingewakabili.

CNN imeongeza kuwa: Jeshi la Israel linatekeleza vitendo hivi katika Ukanda mzima wa Gaza. Hii ni baada ya  wanajeshi wa Israel na raia watano wa Kipalestina kukiri waziwazi.

Mwanajeshi mmoja wa Kizayuni ameiambia CNN kuwa wamekuwa wakiwalazimisha Wapalestina kutangulia mbele katika majengo tofauti kabla yao; na kama itatokea nyumba ikashambuliwa, Wapalestina huwa wa kwanza kupoteza maisha huku wanajeshi wa Israel wakibaki hai. 

Jeshi la Israel linawatumia Wpalestina kama ngao ya binadamu 

Naye Muhammad Said kijana wa Kipalestina aliye na umri wa miaka 20 ambaye ni miongoni mwa Wapalestina waliokamatwa mateka na jeshi la utawala wa Kizayuni ameiambia televisheni ya CNN kuwa jeshi la Israel liliwatumia vijana wa Kipalestina kusafisha maeneo hatari. 

Gazeti la Haaretz linalochapishwa katiak ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) miezi kadhaa iliyopita lilifichua kuwa utawala wa Kizayuni umewatumia raa wa Kipalestina kama ngao ya binadamu katika oparesheni zake dhidi ya Gaza. 

Tags