Israel yashambulia Lebanon, yakiuka makubaliano ya usitishaji vita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i122418-israel_yashambulia_lebanon_yakiuka_makubaliano_ya_usitishaji_vita
Jeshi la Israel limefanya mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya kusini na mashariki mwa Lebanon, huo ukiwa ni ukiukaji mkubwa na wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati yake na nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2025-02-07T07:52:30+00:00 )
Feb 07, 2025 07:52 UTC
  • Israel yashambulia Lebanon, yakiuka makubaliano ya usitishaji vita

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya kusini na mashariki mwa Lebanon, huo ukiwa ni ukiukaji mkubwa na wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati yake na nchi hiyo ya Kiarabu.

Shirika rasmi la habari la Lebanon (NNA) limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi mengi ya anga kwenye miinuko ya milima na eneo moja lililoko katika wilaya ya Baalbek mashariki mwa Lebanon.

Ripoti zinasema kuwa, ndege za kijeshi za Israel zilifanya mashambulizi kadhaa kwenye eneo la Iqlim al-Tuffah kusini mwa Lebanon mwendo wa saa nne na nusu usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, mashambulizi ya anga ya Israel yalilenga miji ya Azzeh na Roumine na eneo karibu na Wadi al-Zahrani. Aidha, ndege za kivita za Israel zimeshambulia kwa mabomu Bonde la Bekaa, mashariki mwa Lebanon karibu na mpaka na Syria.

Israel ililazimika kukubali kusitisha mapigano na Harakati ya Muqawama ya Hizbullah baada ya kupata hasara kubwa kufuatia karibu miezi 14 ya mapigano, na kushindwa kufikia malengo yake katika uvamizi wake dhidi ya Lebanon. Makubaliano ya kusitisha mapigano yalianza kutekelezwa Novemba 27.

Tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano hayo, vikosi vya uvamizi vimekuwa vikiendesha mashambulizi ya karibu kila siku dhidi ya Lebanon kinyume na umapatano hayo, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya anga dhidi ya Beirut, mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu na viunga vyake.