Hamas yaonya juu ya kuvunjika makubaliano ya kusitisha mapigano
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i122752-hamas_yaonya_juu_ya_kuvunjika_makubaliano_ya_kusitisha_mapigano
Msemaji wa Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiisamu ya Palestina HAMAS ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kuvunjika makubaliano ya kusitisha vita kama utawala wa Kizayuni wa Israel utaendelea kufanya vitendo vinavyovunja vipengee vya makubaliano hayo.
(last modified 2025-02-14T23:13:22+00:00 )
Feb 14, 2025 23:13 UTC
  • Hamas yaonya juu ya kuvunjika makubaliano ya kusitisha mapigano

Msemaji wa Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiisamu ya Palestina HAMAS ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kuvunjika makubaliano ya kusitisha vita kama utawala wa Kizayuni wa Israel utaendelea kufanya vitendo vinavyovunja vipengee vya makubaliano hayo.

Katika matukio ya hivi karibuni yanayohusiana na utekelezaji wa makubaliano ya kubadilishana mateka kati ya Muqawama wa Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel, harakati ya Hamas imelazimika kusita kuwasilisha majina ya kundi jingine la mateka wa Israel kutokana na utawala wa Kizayuni kutoheshimu na kuvunja mara kwa mara makubaliano ya kusimamisha vita.

Kabla ya hapo Muqawama wa Palestina ulitangaza kuwa uko tayari kuwaachilia huru mateka wengine wa Israel leo Jumamosi kwa mujibu wa makubaliano ya kubadilishana mateka, lakini kwa sharti kwamba utawala wa Kizayuni nao uheshimu makubaliano hayo. Abu Obeida, Msemaji wa Brigedi za Al-Qassam amesema kuwa, HAMAS itawaachilia huru mateka watatu wa Israeli: Sasha Alexander Trubanov, Sagi Dekel Han na Yair Horn kama sehemu ya awamu ya sita ya mpango wa kubadilishana mateka wa operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa ya Oktoba 7, 2023 lakini kwa sharti kwamba Israel nayo itekeleze makubaliano hayo.

Viongozi wa Hamas wameonya kwamba makubaliano hayo yanaweza kusambaratika ikiwa misafara na magari mazito ya kuondolea vizufusi hayataruhusiwa kuingia kwenye Ukanda wa Ghaza. 

Kwa upande wake, kiongozi mmoja wa Hamas, Osama Hamdan amesema kuwa harakati hiyo iko tayari kuanza awamu ya pili ya mazungumzo siku ya Jumatatu. Duru za habari zimewanukuu wapatanishi wakithibitisha kupata majibu mazuri kutoka pande zote mbili za mazungumzao.