Wakazi wengi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu wanataka Netanyahu ajiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i123698-wakazi_wengi_wa_maeneo_yanayokaliwa_kwa_mabavu_wanataka_netanyahu_ajiuzulu
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni yanaonesha kuwa, Wazayuni walio wengi wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) wanasema kuwa Netanyahu anapaswa kujiuzulu na kukubali kubeba jukumu la kushindwa mkabala wa oparesheni ya wanamapambano wa Palestina ya tarehe 7 Oktoba mwaka 2023.
(last modified 2025-03-09T22:58:13+00:00 )
Mar 09, 2025 22:58 UTC
  • Wakazi wengi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu wanataka Netanyahu ajiuzulu

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni yanaonesha kuwa, Wazayuni walio wengi wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) wanasema kuwa Netanyahu anapaswa kujiuzulu na kukubali kubeba jukumu la kushindwa mkabala wa oparesheni ya wanamapambano wa Palestina ya tarehe 7 Oktoba mwaka 2023.

Uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Demokrasia ya utawala wa Kizayuni unaonyesha kuwa, akthari ya Wazayuni wanaoishi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) wanaamini kuwa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo anapasa kujiuzulu na kubeba dhima ya matukio ya Oktoba 7. 

Uchunguzi huo wa maoni umefanywa na Kituo cha Uchunguzi wa Maoni ya Umma na Sera cha Viterbi kwa kuwashirikisha wanaume na wanawake 759 kuanzia Februari 25 hadi 28 ambapo washiriki waliulizwa ni hatua zipi Netanyahu alipasa kuzichukua?

Aghalabu ya waliohojiwa, asilimia 48, walisema kuwa wanaamini kuwa Waziri Mkuu wa Israel anapaswa kukubali kuwajibika na kujiuzulu haraka iwezekanavyo huku  asilimia 24.5 wakisema kuwa anapasa "kukubali kuwajibika, lakini ajiuzulu baada tu ya kumalizika vita."

Miongoni mwa waliojibu swali hili, asilimia 14.5 walisema kuwa wanaamini kuwa Netanyahu anapasa kukubali masuulia lakini asijiuzulu, na asilimia 10  ya Wazayuni walioshiriki katika uchunguzi huu wa maoni walisema kuwa Netanyahu hapasi kubeba dhima kwa yaliyotokea au kujiuzulu.