Microsoft inashirikiana na Israel katika mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza
Hatua ya Ibtihal Aboussad mhandisi wa nchini Morocco ya kupanda jukwaani na kumshutumu Mustafa Suleyman Mkuu wa Kitengo cha Akili Bandia AI cha Kampuni ya Microsoft imegonga vichwa vya habari duniani.
Mhandisi huyo wa Morocco amemtuhumu Mkuu huyo wa Kitengo cha Akili Bandia cha Microsoft kwa kuiruhusu Israel kutumia akili bandia ya kampuni hiyo kutekeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
Huku suala la kutumiwa akili bandia ya kampuni ya Microsoft katika vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza likiwa limegonga vichwa vya habari duniani; kuna umuhimu pia wa kusikia njia nyingine nyingi ambazo kampuni hiyo imechangia pakubwa kwa utawala huo ghasibu katika historia.
Imeelezwa kuwa, Kampuni ya Highfields Capital Management ya Jonathan Jacobson ina zaidi ya hisa milioni 31 katika kampuni ya Microsoft. Jacobson ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Israeli ya Mafunzo ya Usalama wa Taifa na mdhamini wa taasisi kwa jina la "Birthright Israel Foundation. Yeye pia ni mfadhili wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi na marafiki wa IDF.
Aidha kampuni ya Microsoft inasimamia kampuni kadhaa za teknolojia za utawala wa Kizayuni zilizoanzishwa na wahitimu wa jeshi la Israel kama Aurorato, Adallom, Hexaite na Cyber X.
Jeshi la Israel limedai kuwa lina uwezo wa kutambua maadui wake na kudhibiti roboti na droni na hivyo kuishukuru Microsoft kwa kuipatia kifaa hicho cha utambuzi.