Oktoba 7; Netanyahu aeupuka uwajibikaji huku mgawanyiko ikishadidi Israel
(last modified Wed, 30 Apr 2025 13:36:08 GMT )
Apr 30, 2025 13:36 UTC
  • Oktoba 7; Netanyahu aeupuka uwajibikaji huku mgawanyiko ikishadidi Israel

Miezi 18 baada ya Oktoba 7, 2023, bado serikali ya utawala wa Israel inakabiliwa na taathira za na operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anajaribu kuepuka uwajibikaji huku akijaribu kutupia lawama hii kubwa kwa wengine.

Operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa", iliyoendeshwa na wapiganaji wa Hamas dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mnamo Oktoba 7, 2023, ilikuwa ya kushtukiza kwa mtazamo usalama, na kijeshi, na pia ilikuwa ni kipigo kikubwa cha kijasusi kwa utawala wa  Israel.

Kipigo hiki kilikuwa kikubwa kiasi kwamba Israel ilijaribu kupunguza uzito wake kwa kufanya uhalifu wa kimbari wa kihistoria dhidi ya Gaza, lakini licha ya uhalifu huo, matokeo ya Oktoba 7 hayataondoka kwenye ulingo wa kisiasa wa Israel na yatadumu hata kwa muda mrefu.

Moja ya matokeo muhimu ni kuongezeka kwa migawanyiko ya kisiasa katika mfumo wa utawala wa Israel. Viongozi wa Kizayuni wanarushiana lawama kwa kushindwa kutabiri operesheni ya Oktoba 7, na kwa upande mwingine, wakosoaji wa Benjamin Netanyahu wanatumia tukio hili kama shinikizo dhidi yake.

Kwa msingi huu, Netanyahu anajaribu kujiondoa kwenye uwajibikaji kwa kuwashutumu wakosoaji na wapinzani wake. Katika tukio la hivi karibuni, mivutano kati ya Ronen Bar, mkuu wa Shabak, na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, iko wazi. Shabak ni idara ya ujasusi wa ndani ya Israel.

Bar amekabidhi hati ya kurasa 8 kuhusu operesheni ya Oktoba 7 na alidai kwamba alijulisha viongozi na taasisi zote husika kabla ya shambulio. Amesema pia kwamba Netanyahu alimuomba kutoa taarifa kuhusu waandamanaji walioshiriki katika maandamano. Gazeti la Maariv lilielezea kauli za Ronen Bar kama "bomu la kisheria."

Wapiganaji wa Hamas

Benjamin Netanyahu amesema kauli hizo za Bar ni madai ya uongo. Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kwamba Netanyahu alijibu kwa maandishi ya kurasa 23 kuhusu ripoti ya Ronen Bar na alitaja kauli zote za mkuu huyo wa Shabak kama uongo na zisizo na msingi. Gazeti la Israel Hayom liliripoti kwamba Netanyahu alikabidhi utetezi wake kuhusu matamshi ya Ronen Bar kwa Mahakama Kuu ya Israel na alimtuhumu Bar kwa kusababisha kushindwa kwa kijasusi kubwa zaidi katika historia ya Israel. Netanyahu ammesema kwamba Ronen Bar alikosea kwa namna alivyoshughulikia masuala ya Gaza mwaka 2023 na alitoa matamshi ya uongo kuhusu maandalizi ya kiusalama na juhudi za kuchelewesha kesi ya Waziri Mkuu.

Kauli za Ronen Bar dhidi ya Netanyahu katika Mahakama Kuu ya Israel zinakuja wakati ambapo Netanyahu tayari alikuwa amemfuta kazi kutoka wadhifa wake. Kauli hizi na pia majibu ya Netanyahu yanadhihirisha kwamba operesheni ya Oktoba 7 ilichochea kuongezeka kwa migawanyiko ya ndani katika ya utawala haramu wa Israel, na migawanyiko hii itaendelea kwa muda mrefu.