Unicef: Watoto wa Gaza wana kiu na wana njaa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limeeleza wasiwasi wake kuhusu hali mbaya waliyonayo watu wa Ukanda wa Gaza, hasa watot na kutaka kukomeshwa kmzingiro dhidi ya ukanda huo.
Shirika la Unicef limeripoti kuwa mamia ya malori yaliyobeba bidhaa mbalimbali za mahitaji kwa ajili ya watoto yanasubiri kuingia Ukanda wa Gaza lakini utawala wa Kizayuni umezuia malori hao ya misaada kuingia katika eneo hilo.
Shirika la Unicef limeeleza kuwa: Watoto katika Ukanda wa Gaza ni wagonjwa, wana kiu na wana njaa kwa kukosa chakula. Watoto hao wa Kipalestina wanaishi katika hali ngumu za kibinadamu kutokana na vita.
Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) pia limetahdharisha kuhusu Israel kuendelea kuizingira Gaza na kutangaza kuwa: Hakuna msaada wowote ulioingia Gaza kwa karibu miezi 2 sasa.
Shirika hili la kimataifa, limeashiria hatari inayokaribia ya njaa katika Ukanda wa Gazana kutaka kufunguliwa mara moja kwa vivuko vya mpaka ili kusafirisha misaada muhimu hadi Ukanda huo.
Hii ni katika hali ambayo, duru za kitiba za Palestina leo asubuhi zimetangaza kuwatakriban Wapalestina 31 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo,wanawake na watoto pia ni miongoni mwa waliouliwa shahidi. Nguvu ya hujuma hiyo ya mashambulizi imesabbaisha uharibifu mkubwa katika vitongoji kadhaa vya makazi, na wafanyakazi wa huduma za uokoaji wangali wanafanya juhudi za kuondoa miili ya watu chini ya vifusi vya nyumba zilizoshambuliwa na Israel.