Lieberman: Kamwe hatuwezi kupata amani Israel
Mkuu wa chama cha "Yisrael Beiteinu" amesema kuwa, maadamu utawala unafanya maafa uko madarakani huko Israel, walowezi wa Kizayuni kamwe hawatoonja maisha ya usalama na amani.
Televisheni ya Al Jazeera imemnukuu Avigdor Lieberman akisema hayo wakati alipoonesha hisia zake kutokana na kutozuilika mashambulizi ya makombora ya Yemen yanayoendelea kupiga maeneo muhhimu sana ya Israel katika sehemu mbalimbali za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Amesema: "Maadamu utawala wa maafa unaendelea kutawala Israel, hatutakuwa salama kamwe."
Ikumbukwe kuwa wakati duru za Kizayuni zinapodai zimetungua makombora huwa zinafanya hivyo kujaribu kupunguza hasira za Wazayuni kwani mara nyingi zinakiri kuwa, zinaposema zimetungua hazina maana kwamba zimesambaratisha makombora hayo na kwamba sehemu kubwa sana ya makombora ya Yemen yanapiga maeneo yalikokusudiwa.
Lieberman ameendelea kuushambulia kwa hasira utawala wa Benjamin Netanyahu na kusema kuwa, makombora mawili yaliyorushwa kutoka Yemen katika muda wa saa 24 yamewapeleka mamilioni ya Wazayuni kwenye mashimo na mahandaki.
Redio ya Israel pia imeashiria mashambulizi mapya ya makombora ya wanajeshi wa Yemen katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel na kutangaza kuwa, makombora 25 ya balistiki yamepiga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kutokea Yemen tangu Israel ilipoanzisha upya mashambulizi yake dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ghaza.
Jeshi la Israel ambalo ni maarufu sana duniani kwa kuchuja habari za maafa unazopata utawala wa Kizayuni limedai kuwa limetungua kombora la jeshi la Yemen lakini madai hayo yamekanushwa na Kanali ya 14 ya Televisheni ya Israel ambayo imetangaza kusikika sauti za miripuko mingi kaskazini na katikati mwa ardhi za Palestian zilizopachikwa jina bandia la Israel.
Kama tulivyosema, wakati duru za Kizayuni zinapodai zimetungua makombora huwa zinafanya hivyo kujaribu kupunguza hasira za Wazayuni kwani mara nyingi zinakiri kuwa, zinaposema zimetungua hazina maana kwamba zimesambaratisha makombora hayo na kwamba sehemu kubwa sana ya makombora ya Yemen yanapiga maeneo yalikokusudiwa.