Wapalestina 1373 wauawa shahidi wakisubiri msaada wa chakula Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129082
Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa: Tokea tarehe 27 Mei mwaka huu hadi sasa Wapalestina 1373 wameuliwa shahidi katika Ukanda wa Gaza wakati walipokuwa wakisubiri kugawiwa msaada wa chakula. Waliuliwa shahidi kwa kufyatiliwa risasi na wanajeshi wa Kizayuni.
(last modified 2025-08-03T02:37:19+00:00 )
Aug 03, 2025 02:37 UTC
  • Wapalestina 1373 wauawa shahidi wakisubiri msaada wa chakula Gaza

Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa: Tokea tarehe 27 Mei mwaka huu hadi sasa Wapalestina 1373 wameuliwa shahidi katika Ukanda wa Gaza wakati walipokuwa wakisubiri kugawiwa msaada wa chakula. Waliuliwa shahidi kwa kufyatiliwa risasi na wanajeshi wa Kizayuni.

Ofisi hiyo ya UN imesisitiza kuwa: Watu 859 kati ya mashahidi hao tajwa waliuliwa shahidi katika vituo vya kugawia chakula na wengine 514 katika njia ya misafara ya ugawaji chakula. 

Ripoti ya Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya UN imeeleza kuwa: Tarehe 30 na 30 Julai mwaka huu Wapalestina 105 waliuliwa shahidi katika njia ya misafara ya ugawaji chakula kaskazini mwa Gaza na kusini mwa mji wa Khan-Yunis na katika vituo vya misaada ya mahitaji muhimu yakila siku. Wapalestina wengine 680 walijeruhiwa katika hujuma hiyo. 

Israel imetekeleza mauaji haya ambapo awali jeshi hilo la Kizayuni lilikuwa limetangaza kuwa limepanga kusimamisha shughuli zake za kijeshi kwa masaa kadhaa eti ili kuruhusu misaada ya kibinadamu. 

Kwa mujibu wa ripoti hii, wahanga wengi wa mauaji haya ni watoto na mabarobaro ambao si tishio kwa wanajeshi wa Israel. 

Hii ni katika hali ambayo, mapema leo Taasisi ya Ulinzi wa Mji wa Gaza imetangaza kuwa: Wapalestina 18 wameuliwa shahidi tangu leo asubuhi kufuatia mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza. Aidha miili 13 ya wahanga imeondolewa chini ya vifusi vya nyumba huko mashariki mwa mji wa Gaza unaopatikana kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.