Baada ya kuzuia mashambulizi mengi ya Israel; Yemen yatoa onyo kali kwa Tel Aviv, yasema Wazayuni wajiandae
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i130668-baada_ya_kuzuia_mashambulizi_mengi_ya_israel_yemen_yatoa_onyo_kali_kwa_tel_aviv_yasema_wazayuni_wajiandae
Yemen imetoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni kuhusu uwezekano wa Sana’a kulipiza kisasi vikali dhidi ya mashambulizi ya kinyama ya Tel Aviv huko Yemen.
(last modified 2025-09-11T03:51:02+00:00 )
Sep 11, 2025 03:51 UTC
  •  Baada ya kuzuia mashambulizi mengi ya Israel; Yemen yatoa onyo kali kwa Tel Aviv, yasema Wazayuni wajiandae

Yemen imetoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni kuhusu uwezekano wa Sana’a kulipiza kisasi vikali dhidi ya mashambulizi ya kinyama ya Tel Aviv huko Yemen.

"Hujuma za  kikatili za Wazayuni dhidi ya nchi yetu zimefeli, na Wazayuni wote wanapaswa kujiandaa kwa kuwa jibu na ulipizaji kisasi dhidi yao linakuja," amesema Mahdi al-Mashat, Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen  katika taarifa yake siku ya Jumatano.

Amesema kuwa uchokozi wa Wazayuni utaipatia Yemen fursa kubwa ya kujibu hujuma za Israel kwa nguvu zote. 

Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ameeleza haya baada ya watu 35 kuuawa na wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa katika mashambulizi ya ndege za kivita za Israel katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a na katika mkoa wa al Jawf kaskazini mwa nchi hiyo. 

Kwa upande wake Jeshi la Yemen lilikabiliana na ndege vamizi za Israel kwa kuvurumisha makombora ya kutoka ardhini kuelekea angani. 

Brigedia Jenerali Yahya Saree Msemaji wa jeshi la Yemen ametoa taarifa na kupongeza  hatua iliyochukuliwa na jeshi na kueleza kuwa vikosi vya ulinzi vimefanikiwa kuwazimisha wanajeshi wa Israel kuondoka kabla ya kufanya uchokozi dhidi ya nchi hiyo. Amesema sehemu kubwa ya mashambulizi ya Israel yamesambaratishwa.