Lavrov: Lengo la Israel ni kudhoofisha uwezekano wa kuundwa taifa huru la Palestina
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesisitiza kwamba, hatua za utawala wa Kizayuni zinaonyesha njama zake za kudhoofisha mkakati wa kuundwa "Nchi ya Palestina".
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia Sergei Lavrov aliyehudhuria mkutano wa 8 wa mawaziri wa Mazungumzo ya Kimkakati kati ya Russia na nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba huko Sochi, na kando ya mkutano huo, alikutana na Sultan bin Saad Al-Muraikhi, Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Qatar.
Lavrov alisema: Mivutano ya kijeshi na kisiasa katika Mashariki ya Kati imeongezeka sana baada ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas nchini Qatar.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza kuwa, hatua za utawala wa Kizayuni zinaonyesha nia yake ya kudhoofisha uwezekano mkubwa sana wa kuundwa taifa la Palestina.
Lavrov pia alisema katika Mazungumzo ya Kimkakati ya Russia na GCC huko Sochi: "Mikutano yetu hii leo inafanyika huku kukiwa na ongezeko kubwa la mivutano ya kijeshi na kisiasa katika Asia Magharibi kutokana na mashambulizi ya makombora ya Israel na mashambulizi ya mabomu huko Doha, Qatar, Septemba 9."
Lavrov alimalizia kwa kusisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, vitendo vya Israel vinaonyesha nia yake ya kudhoofisha uwezekano wa kuunda taifa la Palestina.