Rais wa Bolivia: Marekani na Israel ‘zinatekeleza mauaji ya kimbari’ Gaza
-
Rais wa Bolivia, Luis Arce
Rais wa Bolivia, Luis Arce, amekemea vikali Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kusababisha maumivu na vifo duniani kote na “kutekeleza mauaji ya kimbari” katika Ukanda wa Gaza uliokuwa umezingirwa.
Akiwa anahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Alhamisi, Arce alizitambulisha Marekani na Israel kama waenezaji vita wenye “hamu ya kupindukia” ya kusababisha mateso na vifo kote duniani.
“Tishio la kifo pia lipo kote Mashariki ya Kati,” alisema Arce, akirejelea vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza, kwa ushiriki wa Israel na Marekani. Amesema tawala hizo mbili zinataka kuharakisha kuondoshwa kwa watu wa Palestina katika muda mfupi kabisa.
Mashambulizi dhidi ya ukanda ambao umezingirwa yamesababisha hadi sasa vifo vya Wapalestina zaidi ya 65,500, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Kiongozi huyo wa Bolivia pia amelaani uchochezi wa hivi karibuni wa Washington dhidi ya Venezuela, huku akisisitiza kuwa “tishio la kifo linavizia Amerika ya Kusini na Karibiani.”
Arce alisema Kamandi ya Kusini ya Jeshi Marekani imejipanga katika eneo hilo ikiwa na “uwezo wa kivita,” ikiwemo makombora, ndege, helikopta na manowari.
Amepinga madai ya Marekani kuwa eti inapambana na “biashara haramu ya dawa za kulevya na uhalifu uliopangwa” kama wa uwongo, akisema, “kama ingekuwa kweli, ingeanza kukabiliana na masuala haya katika nchi yake yenyewe.”
Alibainisha kuwa uwepo wa majeshi ya Marekani katika eneo hilo ni kisingizio cha kuingilia Venezuela, nchi ambayo rasilimali muhimu sana za asili, hasa mafuta,” kwa njia ya “kivita na mbinu za ukoloni.”
Arce alisema kuwa dunia inaendelea kubeba madhara ya vita, vizuizi na vikwazo vya upande mmoja ambavyo vinapingana na kanuni kuu ambazo Umoja wa Mataifa umejengwa juu yake.
Rais wa Bolivia alitoa mfano wa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Cuba, akisema vikwazo hivyo vimetokana na “madola ya kibeberu kupinga mapinduzi ya kwanza ya kisoshalisti katika eneo,” na kusababish upotevu wa mabilioni ya fedha kutokana na hatua ya upande mmoja ya serikali ya Marekani iliyoendelea kwa zaidi ya miongo sita.