Greta Thunberg: Israel ilinitesa na wanaharakati wengine wa Gaza Flotila
Mwanaharakati wa masuala ya hali ya hewa wa Uswidi, Greta Thunberg ameeleza kuwa yeye na wanaharakati wengine wa msafara wa Sumud au Global Sumud Flotilla uliokuwa ukielekea Gaza waliteswa na kunyanyaswa walipokuwa wakishikiliwa katika magereza ya Israel baada ya jeshi la wanamaji la utawala huo kuwatia nguvuni katika maji ya kimataifa.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari mjini Stockholm Sween, Thunberg amesema kuwa yeye na wanaharakati wengine kadhaa walitekwa nyara na kuteswa na jeshi la Israel hata hivyo hakutoa maelezo zaidi.
Aliposhinikizwa na waandishi wa habari, Bi Greta Thunberg alisema: Watu wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel wananyimwa maji safi na huduma muhimu za tiba.
Mwanaharakati huyo raia wa Sweden ametilia mkazo kuhusu masaibu na mateso wanayopitia kila siku raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro wa Israel.
Thunberg alikuwa sehemu ya msafara wa kimataifa wa Sumud; kundi la meli za kimataifa zilizokuwa zikisafari kuelekea Gaza ili kuwasilisha misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza na kuweka wazi mateso wanayopitia wakazi wa eneo hilo ambao wameathiriwa na njaa ya makusudi iliyosababishwa na utawala wa Kizayuni.
Utawala wa Kizayuni juzi Jumatatu ulimuachia huru mwanaharakati huyo wa Sweden ambaye alitiwa nguuni na utawala huo pamoja na wanaharakati wengine wa msafara huo wa kimataifa wapatao 478.
Israel inadai kuwa msafara wa kimataifa wa Flotila ni propaganda za kimataifa zenye lengo la kuinufaisha harakati ya Hamas na utawala huo mwezi Juni mwaka huu ulimtia mbaroni mbaroni Thunberg katika hujuma yake nyingine sawa na hivi majuzi.