Nchi zilizosaini mkataba wa kuuza silaha zimetakiwa kuacha kuiuzia silaha Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i13759-nchi_zilizosaini_mkataba_wa_kuuza_silaha_zimetakiwa_kuacha_kuiuzia_silaha_saudia
Shirika kubwa la uuzaji silaha limezishambulia kwa maneno nchi na pande zilizosaini Mkataba wa Uuzaji Silaha (ATT), ikiwemo Marekani kwa kuendelea kuiuzia Saudi Arabia silaha, likisema kuwa nchi hizo zinapaswa ziache kufanya hivyo kwa kuwa silaha hizo zinatumika dhidi ya raia nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 22, 2016 10:37 UTC
  • Nchi zilizosaini mkataba wa kuuza silaha zimetakiwa kuacha kuiuzia silaha Saudia

Shirika kubwa la uuzaji silaha limezishambulia kwa maneno nchi na pande zilizosaini Mkataba wa Uuzaji Silaha (ATT), ikiwemo Marekani kwa kuendelea kuiuzia Saudi Arabia silaha, likisema kuwa nchi hizo zinapaswa ziache kufanya hivyo kwa kuwa silaha hizo zinatumika dhidi ya raia nchini Yemen.

Anna Macdonald, Mkurugenzi wa Shirika hilo la kudhibiti silaha amesema kuwa kila siku wanashuhudia athari kubwa za uuzaji silaha na zana za kijeshi zinazotumika dhidi ya raia huko Yemen. Ameongeza kuwa nchi kama Ufaransa, Uingereza na Marekani zimekuwa zikipuuza sheria za kimataifa waziwazi kwa kuendelea kuiuzia Saudia silaha za mabilioni ya dola.

Raia wasio na hatia wanauliwa ovyo na ndege za Saudia huko Yemen

Saudi Arabia ilianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen mwezi Machi mwaka jana na kisha nchi hiyo ikaanzisha mashambulizi ya ardhini ili kuidhoofisha Harakati ya Ansarullah iliyoko madarakani na wafuasi wake ili kumrejesha madarakani Abd Rabbuh Mansour Hadi, Rais wa Yemen aliyejiuzulu. Karibu watu elfu kumi, wengi wakiwa ni raia wameuliwa katika uvamizi wa kijeshi wa utawala wa Aal Saud ambao ulifanyika nchini humo bila ya idhini yoyote ya kimataifa.

Uharibifu uliofanywa na ndege za kivita za Saudia Yemen

Wakati huo huo mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu na taasisi za kutetea haki za binadamu zenye wawakilishi wake huko Yemen zimethibitisha kesi nyingi za mashambulizi ya Saudia yanayowalenga raia nchini humo.