Basi lililowabeba mahujaji wa Algeria lawaka moto
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i14254-basi_lililowabeba_mahujaji_wa_algeria_lawaka_moto
Katika kuendelea na kukaririwa matukio yanayohusiana na ibada ya Hija huko Saudi Aarbia, basi moja lililokuwa limewabeba mahujaji wa Algeria wakitokea Madina na kuelekea mjini Makka limewaka moto.
(last modified 2026-05-19T09:45:50+00:00 )
Aug 30, 2016 03:04 UTC
  • Basi lililowabeba mahujaji wa Algeria lawaka moto

Katika kuendelea na kukaririwa matukio yanayohusiana na ibada ya Hija huko Saudi Aarbia, basi moja lililokuwa limewabeba mahujaji wa Algeria wakitokea Madina na kuelekea mjini Makka limewaka moto.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria jana alasiri iliripoti kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme ndani ya basi lililokuwa limewabeba mahujaji wa nchi hiyo na kwamba hakuna hujaji aliyedhurika na moto huo. Hi ni katika hali ambayo zimesalia siki kadhaa tu hadi kuanza marasimu ya Ibada ya Hija huko Saudia. Mahujaji 65 wa Algeria tarehe 18 mwezi Juni mwaka huu pia walilazwa katika hospitali ya Mfalme Faisal na Mfalme Abdulaziz huko Saudi Arabia baada kudhurika na chakula. Suala la kuandaa marasimu ya ibada ya Hija na kuwadhaminia mahujaji usalama wao linatiliwa mkazo na fikra za waliowengi khususan baada ya kupoteza maisha mwaka jana mahujaji 108 na wengine 238 kujeruhiwa kufuatia kuanguka winchi katika Masjidul Haram. Mmoja wa mahujaji aliyeaga dunia na majeruhi wawili walikuwa raia wa Algeria; ambao hadi sasa wanasubiri kulipwa fidia. Aidha tukio chungu na la kuhuzunisha lililotokea Mina katika Hija ya Mwaka jana  lilisababisha vifo vya mamia ya mahujaji kutoka pembe mbalimbali duniani khususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Algeria ilipoteza mahujaji wake 50 katika tukio la kukanyagana la Mina.

Tukio chungu la Mina mwaka jana ambapo mamia ya mahujaji waliaga dunia