Utawala wa Kizayuni washambulia kwa mizinga Ukanda wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i14725-utawala_wa_kizayuni_washambulia_kwa_mizinga_ukanda_wa_ghaza
Kikosi cha mizinga cha utawala wa Kizayuni wa Israel kimefanya mashambulizi katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza huko Palestina.
(last modified 2026-05-10T14:24:40+00:00 )
Sep 06, 2016 02:58 UTC
  • Utawala wa Kizayuni washambulia kwa mizinga Ukanda wa Ghaza

Kikosi cha mizinga cha utawala wa Kizayuni wa Israel kimefanya mashambulizi katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza huko Palestina.

Shirika la habari la Fars limeripoti kuwa, kikosi hicho cha wanajeshi katili wa Israel mapema leo asubuhi kimeshambulia mara tano maeneo ya kaskazini mwa ukanda huo kama vile katika kituo kimoja cha kijeshi cha "Saraya al Quds," tawi la kijeshi la Jihadul Islami na kituo cha kijeshi kiitwacho "Felestin" pamoja na eneo moja la makazi ya watu, na maeneo kadhaa ya wazi huko Bait Lahya, kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.

Wahanga wakubwa wa mashambulizi ya kikatili ya Israel huko Ghaza, ni watoto maasumu

 

Mashambulizi hayo hayakusababisha hasara zozote za roho za watu, lakini yamefanya uharibifu mkubwa.

Vile vile wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wamevamia maeneo kadhaa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwateka nyara raia wa Kipalestina bila ya sababu yoyote, kwa madai kuwa wanajeshi hao wa utawala wa Kizayuni wameshambuliwa kwa risasi na Wapalestina wenye silaha.