Russia yatahadharisha kuhusu kuchelewa kuanza tena mazungumzo ya Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15274-russia_yatahadharisha_kuhusu_kuchelewa_kuanza_tena_mazungumzo_ya_syria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa kuchelewa kuanza tena mazungumzo ya Syria ni jambo lisilokubalika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2016 23:44 UTC
  • Russia yatahadharisha kuhusu kuchelewa kuanza tena mazungumzo ya Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa kuchelewa kuanza tena mazungumzo ya Syria ni jambo lisilokubalika.

Sergei Lavrov amesema leo katika mkutano na waandishi wa habari huko Moscow akiwa pamoja na Jean Asselborn Waziri mwenzake wa Luxembourg kwamba Russia imemtaarifu Stephen de Mistura Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Syria kuwa kuendelea kucheleweshwa kuanza tena mazungumzo ya Syria ni jambo lisilokubalika.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia (kulia) akiwa na mwenzake wa Luxembourg mjini Mscow 

Lavrov ameongeza kuwa Moscow iko tayari kuwa mwenyeji wa kikao na Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni na kwamba, Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri pia anaunga mkono kikao hicho. Waziri wa Mambo ya Nje wa Luxembourg pia amepongeza juhudi za Russia za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria na akasema, kufikiwa makubaliano ya usitishaji vita kutaanda uwanja wa kuanza tena mazungumzo ya Geneva kuhusu Syria.