Kushtadi jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina
Ripoti zinaarifu kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umezidisha jinai na vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya raia wa Palestina na katika fremu hiyo Wapalestina wanne wameuliwa shahidi kwa kupigwa risasi.
Kuuliwa shahidi Wapalestina hao wanne, kunaifanya jumla ya Wapalestina waliouawa shahidi katika Intifadha ya Quds kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa kufikia 244. Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina yamekuwa yakishuhudia malalamiko na maandamano makubwa ya Wapalestina wanaopinga siasa za kichokozi za utawala wa Kizayuni za kutaka kubadilisha utambulisho wa Baitul Muqaddas na kuandaa mpango wa kugawa Masjidul Aqsa. Siasa hizo za kichokozi za utawala wa Kizayuni ndiyo sababu ya kuanza tena Intifadha ya Quds.
Viongozi wa Israel wamezidisha mauaji dhidi ya Wapalestina katika hali ambayo sera za kutumia mabavu na za kichokozi za utawala huo zinazidisha idadi ya mashahidi wa Kipalestina. Matukio ya Palestina yanadhihirisha ukubwa wa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni unaoendelea kutenda aina mbalimbali ya jinai na kuwakandamiza raia wa Palestina.
Utawala wa Kizayuni umeweka katika ajenda yake suala la kuwakandamiza Wapalestina huku viongozi wa Israel, akiwamo Avigdor Lieberman Waziri wa Vita wa utawala huo, akisisitiza kushadidishwa hatua hizo za kuwakandamiza Wapalestina.
Lieberman ametangaza kuwa kubomolewa nyumba za raia wa Palestina na kufukuzwa katika ardhi za zao hususan familia za wale waliotekeleza mashambulizi dhidi ya Uzayauni maghasibu ni moja ya njia zilizotumiwa na Israel kwa ajili ya kuzidisha mashinikizo dhidi ya wananchi wa Palestina. Lieberman amesisitiza kuwa, mbali na kuuliwa wanaharakati wa Kipalestina, suala la kuuliwa vingozi wa harakati za Kipalestina akiwemo Ismail Hania na Khalid Mash'al pia linapasa kuwekwa katika ajenda ya Israel. Wakati huo huo ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa kumeanza duru mpya ya misimamo ya kibaguzi na kigaidi ya utawala wa kizayuni; suala ambalo linadhihirisha wazi zaidi namna misingi ya utawala huo ilivyojengeka katika sera za utumiaji mabavu.
Kwa kuzidisha jinai zake dhidi ya raia wa Palestina, utawala wa Kizayuni unataka kuwalazimisha raia hao wasalimu amri mbele ya matwaka yao ili washindwe kuendeleza mapambano ya dhidi ya Wazayuni maghasibu. Hakuna shaka kuwa katika muda wa miaka 68 ya kukaliwa kwa mabavu Palestina, utawala wa Kizayuni Usrael uliratibu mauaji ya Wapalestina na kuliweka suala hilo katika ajenda ya viongozi na waasisi wa Israel. Imefahamika kuwa mauaji hayo yaliyopangiliwa na Israel kwa malengo maalumu yaliandaliwa tangu awali kwa uungaji mkono wa Uingereza na Marekani na kwa kutegemea taasisi za kigaidi za Kizayuni kama vile Irgun, Haganah na Ishten. Taasisi hizo za kigaidi zilikuwa zikipatiwa mafunzo huko Uingereza na kufanya mauaji ya Wapalestiina katika ameneo ya umma kama katika masoko, migahawani na ndani ya mabasi, lengo lilikuwa kuzusha anga ya ukosefu wa amani na hofu ili kwa njia hiyo raia wa Palestina walazimike kuyahama makazi yao na kwenda nje ya Palestina.
Jinai kama hizo zinadhihirisha jinsi sera za utumiaji mabavu na kupenda kujitanua za utawala wa Kizayuni wa Israel zilivyotokana na imani na mafunzo ya utawala huo wa kibaguzi; jambo ambalo limeshuhudiwa katika mauaji makubwa ya Wapalestina katika wiki kadhaa za hivi karibuni.
Duru mpya ya vitisho, mashambulizi na vitendo vya kujitanua vya utawala wa Kizayuni huko palestina yanafanyika sambamba na kuzidishwa misaada ya kijeshi ya Marekani kwa utawala huo haramu, hatua ambayo inachukuliwa kuwa ni sawa na kupewa baraka utawala huo na Marekani ili kuzidisha hujuma na ukatili wake katika eneo la Mashariki ya Kati.