Israel yataka kupitisha sheria ya kuwanyonga mateka wa Kipalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15736-israel_yataka_kupitisha_sheria_ya_kuwanyonga_mateka_wa_kipalestina
Waziri mmoja wa utawala wa Kizayuni wa Israel amemtaka Waziri wa Vita wa utawala huo haramu Avigdor Lieberman atimize ahadi aliyotoa ya kupitisha sheria ya kuwanyonga Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala huo.
(last modified 2026-05-13T14:18:38+00:00 )
Sep 21, 2016 00:06 UTC
  • Israel yataka kupitisha sheria ya kuwanyonga mateka wa Kipalestina

Waziri mmoja wa utawala wa Kizayuni wa Israel amemtaka Waziri wa Vita wa utawala huo haramu Avigdor Lieberman atimize ahadi aliyotoa ya kupitisha sheria ya kuwanyonga Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala huo.

Uri Ariel, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mashambani wa utawala haramu wa Israel alimtaka Lieberman atimize ahadi hiyo ya kupitisha sheria ya kuwanyonga Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya Israel, wakati waziri huyo wa vita wa utawala wa Kizayuni alipokuwa akihutubia hapo jana katika kituo cha utafiti wa usalama wa ndani wa Israel mjini Tel Aviv .

Ariel alidai kwamba Israel haina taarifa zozote kuhusu hatima ya askari wake waliotoweka Ukanda wa Gaza, hali ya kuwa mateka wa Kipalestina wanaishi kwenye mazingira yanayofanana na ya kambini.

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni, Avigdor Lieberman

Mwezi Februari 2015, Avigdor Lieberman, kiongozi wa chama cha Kizayuni cha mrengo wa kulia cha "Israel Nyumba Yetu" aliahidi kuwa hatua ya kwanza itakayochukuliwa na chama chake endapo kitashinda uchaguzi wa bunge la Kizayuni la Knesset ni kupitisha sheria ya kuwanyonga mateka wa Kipalestina.

Utawala haramu wa Israel umekuwa ukifanya juu chini kupoka kikamilifu haki za Wapalestina, ambapo mbali na kukataa kuwaachiliwa huru Wapalestina unaowashikilia kwenye magereza yake yenye mazingira mabaya na ya kuogofya unaendelea kuwateka nyara Wapalestina wengine zaidi na kuwatia korokoroni.

Hivi sasa kuna zaidi ya Wapalestina 7,000 wanaoishi kwenye hali mbaya katika jela za utawala haramu wa Israel.../