Madola ya Magharibi yanatumia vibaya hali ya kibinadamu Syria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid al-Muallem amekosoa baadhi ya madola ya Magharibi na Mashariki ya Kati kwa kutumia vibaya masaibu ya kibinadamu ya Wasyria kufikia malengo yao ya kisiasa.
Akihutubu katika kikao cha 71 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Jumamosi, Muallem amesema Syria imekuwa ikilaumiwa kwa hali mbaya ya kibinadamu nchini humo pamoja na kuwa baadhi ya madola yanapendelea hali hiyo ili kufikia malengo yao.
Ameongeza kuwa nchi za Magharibi zinaituhumu serikali ya Syria kwa kusababisha njaa kwa makusudi katika hali mbayo nchi hizo za Magharibi ndizo zinazowaunga mkono magaidi wa Syria na kuwatumia wanadamu kama ngao ya kivita.
Muallem amesema serikali ya Syria itafanya kila iwezalo kumaliza masaibu ya wananchi na kuhakikisha wanapata tena hadhi na heshima.
Katika sehemu nyigine ya hotuba yake, Muallem amesema Syria imekuwa ikikabiliana na ugaid wa Israel kwa muda mrefu wakati utawala huo ulipokalia kwa mabavu Miinuko ya Golan mwaka 1967.
Ameongeza kuwa Israel inawaunga mkono magaidi nchini Syria kupitia miinuko ya Golan. Muallem pia amesema uungaji mkono wa Marekani kwa magaidi wa kitafkiri wa ISIS au Daesh na makundi mengine ya kigaidi ni kizingiti kikubwa katika kusitishwa vita nchini humo.