Saudia yasisitiza kuwapatia silaha magaidi nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1630-saudia_yasisitiza_kuwapatia_silaha_magaidi_nchini_syria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ametaka magaidi walioko nchini Syria waimarishwe kwa silaha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 20, 2016 23:17 UTC
  • Saudia yasisitiza kuwapatia silaha magaidi nchini Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ametaka magaidi walioko nchini Syria waimarishwe kwa silaha.

Adel al-Jubeir ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Kijerumani la Der Spiegel na kutamka kuwa makundi yanayobeba silaha (magaidi) lazima yapatiwe makombora ya kutungulia ndege ili mlingano wa nguvu za kijeshi nchini humo uwe ni kwa manufaa ya makundi hayo.

Al-Jubeir ameongeza kuwa endapo yatakuwa na silaha za kisasa, makundi hayo yanaweza kuishinda serikali ya Syria.

Utawala wa Aal-Saud umekuwa ukiyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria na kuyasaidia kwa fedha na silaha.

Wakati huohuo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema uchokozi na uvamizi wowote utakaofanywa dhidi ya ardhi ya Syria utakabiliwa na jibu kali la Damascus.

Faisal al-Miqdad amesisitiza kuwa serikali ya Damascus inalinda mamlaka ya kujitawala ya ardhi yote ya nchi hiyo kwa kukabiliana na maadui na magaidi; na haitoruhusu Uturuki au nchi nyengine yoyote ile ikiuke mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo.../