Mahmoud Abbas azidi kulaumiwa kwa kushiriki maziko ya Peres
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16414-mahmoud_abbas_azidi_kulaumiwa_kwa_kushiriki_maziko_ya_peres
Makundi mbalimbali ya Palestina yameendelea kumlaumu Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa kushiriki kwenye maziko ya nduli wa Israel, Shimon Peres, rais wa zamani wa utawala wa Kizayuni.
(last modified 2026-05-10T14:24:40+00:00 )
Oct 01, 2016 00:52 UTC
  • Mahmoud Abbas azidi kulaumiwa kwa kushiriki maziko ya Peres

Makundi mbalimbali ya Palestina yameendelea kumlaumu Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa kushiriki kwenye maziko ya nduli wa Israel, Shimon Peres, rais wa zamani wa utawala wa Kizayuni.

Ili kupunguza lawama hizo, harakati ya Fat'h ya Mahmoud Abbas imejaribu kuhalalisha jambo hilo kwa kudai kuwa, hatua ya Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kushiriki kwenye maziko hayo ni kuonesha nia njema.

Shirika la habari la Xinhua limemnukuu Munir al Yaakub, mmoja wa viongozi waandamizi wa harakati ya Fat'h katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan akisema jana (Ijumaa) kuwa, hatua ya Mahmoud Abbas ya kushiriki katika maziko ya Peres ni kufikisha ujumbe wa amani kwa walimwengu.

Picha iliyopigwa kutoa katika video, inamuonyesha Mahmoud Abbas akisalimiana na Benjamin Netanyahu katika maziko wa Shimon Peres

 

Pembeni mwa maziko hayo, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amefanya mazungumzo na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ambaye mikono yake imejaa damu za Wapalestina wasio na hatia.

Makundi mengi ya Palestina yamekasirishwa mno na kitendo hicho na yamekilaani vikali. Harakati ya Mapambano ya Palestina HAMAS imesema, kushiriki kwenye maziko hayo ni sawa na kukanyaga kijeuri damu za mashahidi wa Palestina zilizomwagwa na Shimon Peres.

Naye Sheikh Khadhar Adnan, mmoja wa viongozi wa harakati ya Jihadul Islami amesema, kitendo cha baadhi ya viongozi wa Palestina cha kushiriki kwenye maziko ya Peres ni sawa na kutangaza kushikamana kwao na makatili wanaomwaga ovyo damu za Wapalestina na kuzikalia kwa mabavu ardhi zao.