Ofisa wa Palestina akamatwa kwa kumkosoa Mahmoud Abbas
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16498-ofisa_wa_palestina_akamatwa_kwa_kumkosoa_mahmoud_abbas
Vikosi vya usalama vya Palestina vimemkamata ofisa mmoja wa jeshi baada ya kukosoa hatua ya Mamhoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhudhuria mazishi ya Shimon Peres, rais wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-05-13T18:57:29+00:00 )
Oct 02, 2016 04:37 UTC
  • Ofisa wa Palestina akamatwa kwa kumkosoa Mahmoud Abbas

Vikosi vya usalama vya Palestina vimemkamata ofisa mmoja wa jeshi baada ya kukosoa hatua ya Mamhoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhudhuria mazishi ya Shimon Peres, rais wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la Ma’an limeripoti, Osama Mansour Abu Arab ambaye ni mshirikishi wa Vikosi vya Usalama wa Taifa vya Palestina anayehusika na masuala ya Israel amekamatwa mjini Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, baada ya kueleza ghadhabu zake katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook akikosoa hatua ya Mahmoud Abbas kuhudhuria mazishi ya Peres.

 Mahmoud Abbas (Kushoto) akisemezana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Katika chapisho hilo, Abu Arab aliandika kuwa "Haingii akilini kwa Mahmoud Abbas kuhudhuria maziko na kutoa salamu za rambirambi kwa muasisi wa upanuzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni."

Makundi mbalimbali ya Palestina yameendelea kumlaumu Mahmoud Abbas, kwa kushiriki kwenye maziko ya Peres, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Mahmoud Abbas na Shimon Peres

Harakati ya Mapambano ya Palestina HAMAS imesema, kushiriki kwenye maziko hayo ni sawa na kukanyaga damu za mashahidi wa Palestina zilizomwagwa na Shimon Peres.