Vikosi vya kujitolea vya Wayemeni vyajibu jinai za Saudia
Jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen vimefanya oparesheni kusini mwa Saudi Arabia na kuuwa na kuwajeruhi wanajeshi kadhaa wa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Yemen imetangaza leo Jumapili kuwa jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananch iwa Yemen vimezishambulia kambi mbili za kijeshi za Saudi Arabia mkoani Jizan na kuuuwa wanajeshi 25 wa nchi hiyo, ikiwa ni katika kujibu mauaji ya umati ya raia wa Yemen yaliyofanywa na muungano vamizi wa Saudi Arabia huko Sana'a jana jioni.
Makumi ya wanajeshi wa Saudia wamejeruhiwa pia katika oparesheni hiyo. Wakati huo huo George Khouri Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayohusika na Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Yemen amesisitiza mwishoni mwa maandamano makubwa ya leo ya maelfu ya wananchi wa Yemen mjini Sana'a yaliyopewa ajina la "Hasira za Volkano" kuwa mashirika ya kibiandamu yangali yako nchini humo na kwamba yupo pamoja na wananchi wa Yemen katika maafa hayo ya kuhuzunisha.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ametaka kufanyike uchunguzi haraka iwezekanavyo na wa wazi kuhusu jinai za umwagaji damu zilizofanywa na Saudi Arabia huko Sana'a mji mkuu wa Yemen na kutaka pia kusimamishwa vita nchini humo haraka iwezekanavyo. Ndege za kivita za Saudi Arabia jana ziliushambulia ukumbi mmoja mjini Sana'a Yemen ambako watu wa matabaka mbalimbali walikuwa wamekusanyika katika maziko na kuua watu 140 na kujeruhi wengine 525.