Kiwango cha umasikini Palestina kimeongezeka
Taasisi ya haki za binadamu ya Al-Mizaan imetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndio msababishaji mkuu wa ongezeko la umasikini walionao Wapalestina.
Katika ripoti yake kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Umasikini, Al-Mizaan imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia hali ya umasikini waliyonayo Wapalestina na kutangaza kuwa sera za utawala wa Kizayuni wa Israel katika miaka ya hivi karibuni zimesababisha kuongezeka kiwango cha umasikini ndani ya jamii ya Wapalestina.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo ya kutetea haki za binadamu ya Palestina utawala haramu wa Kizayuni umesababisha kushtadi umasikini Palestina kutokana na kuendeleza mzingiro wake, kubomoa taasisi za miundomsingi na kuangamiza miundo ya viwanda, kilimo na biashara ya Wapalestina.
Ripoti ya taasisi ya Al-Mizaan aidha imeashiria sababu zingine za kuongezeka umasikini katika jamii ya Wapalestina ikiwa ni pamoja na vizuizi vinavyowekwa na utawala haramu wa Israel katika mabadilishano ya bidhaa baina ya Palestina na nje ya mipaka ya ardhi hiyo, udhibiti wa vyanzo vya maji, kuteketeza mazao ya kilimo katika mashamba ya Wapalestina, kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kujenga ukuta wa kibaguzi kwa madhumuni ya kushadidisha mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza na Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.
Katika miaka ya karibuni hali ya Ukanda wa Gaza imekuwa mbaya zaidi kulinganisha na Ufukwe wa Magharibi ambapo baada ya vita vya mwaka 2014 vya Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia asilimia 43 na kukadiriwa kuwa kiwango cha juu zaidi duniani.
Takribani mwaka wa kumi sasa utawala wa Kizayuni umeshadidisha mzingiro wake dhidi ya Ukanda wa Gaza, katika Plaestina inayokaliwa kwa mabavu.../