Watu elfu tisa wamekuwa wakimbizi Mosul
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18178-watu_elfu_tisa_wamekuwa_wakimbizi_mosul
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa watu karibu elfu tisa wamekuwa wakimbizi katika mji wa Mosul nchini Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 26, 2016 03:31 UTC
  • Watu elfu tisa wamekuwa wakimbizi Mosul

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa watu karibu elfu tisa wamekuwa wakimbizi katika mji wa Mosul nchini Iraq.

Stephen Dujaric ameeleza kuwa idadi ya wakimbizi waliopo katika mji wa Mosul, ambao wanajeshi wa Iraq wameanza kufanya oparesheni ya kuukomboa kutoka mikononi mwa wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la kigaidi la Daesh, imefikia karibu elfu tisa. 

Dujaric ameongeza kuwa, familia ambazo ziliukimbia mji wa Mosul kutokana na kuendelea oparesheni za kuukomboa mji huo zinaishi katika hali mbaya na zinahitaji misaada ya kibinadamu.

Wanaume, wanawake na watoto wa Kiiraqi wakiukimbia mji wa Mosul

Stephen Dujaric amesema kuwa Umoja wa Mataifa umepata taarifa kwamba magaidi wa Daesh  wanawatumia kwa makusudi raia huko Mosul kama ngao ya binadamu. Oparesheni ya kuukomboa mji wa Mosul ilianza tarehe 17 mwezi huu kwa amri ya Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al Abadi. Maelfu ya vikosi vya jeshi na polisi ya Iraq wakishirikiana na vikosi vya kujitolea vya Wairaqi na wapiganaji wa Pishmerga hivi sasa wanasonga mbele katika maeneo tofauti katika mji wa Mosul ambacho ni kitovu cha harakati za kundi la Daesh.