Sarkozy: Iran ina nafasi kuu katika kupatikana amani Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18775-sarkozy_iran_ina_nafasi_kuu_katika_kupatikana_amani_mashariki_ya_kati
Nicolaus Sarkozy rais wa zamani wa Ufaransa amesisitiza umuhimu wa nafasi ya Iran katika kupatikana amani katika eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2026-09-03T12:21:49+00:00 )
Nov 04, 2016 04:03 UTC
  • Sarkozy: Iran ina nafasi kuu katika kupatikana amani Mashariki ya Kati

Nicolaus Sarkozy rais wa zamani wa Ufaransa amesisitiza umuhimu wa nafasi ya Iran katika kupatikana amani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Sarkozy aliyasema hayo katika mdalaho wa pili wa wagombea saba wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Ufaransa uliofanyika jana usiku kwa ajili ya kumuainisha mgombea rasmi wa chama hicho atakayepeperusha bendera katika uchaguzi ujao wa Rais ulifanyika jana usiku. Rais wa zamani wa Ufaransa aliashiria nafasi kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia na kueleza kuwa, iwapo mtu anafikiri kwamba anaweza kurejesha amani katika maeneo ya kando kando ya Mediterania bila ya kushirikishwa Tehran na Moscow, mtu huyo atakuwa yuko katika makosa kikamilifu.

Wagombea saba wa chama cha Republican cha Ufaransa wakiwa katika mdahalo

Sarkozy ameongeza kuwa, siasa zake za nje pia zinatoa kipaumbele kwa  suala hilo.

Katika mdahalo huo wa jana usiku, wagombea saba wa chama cha Republican kwa muda wa masaa mawili na nusu waliwasilisha mipango na sera zao kwa wananchi na kukosoa utendaji wa Rais wa nchi hiyo kwa miaka mitano iliyopita.

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa ndani wa chama cha mrengo wa kulia kati umepangwa kufanyika siku 17 zijazo. Nicolaus Sarkozy rais wa zamani wa Ufaransa, Francois Fillon na Len Allain Juppe, mawaziri wakuu wa zamani, Bruno Le Maire, Nathalie Morizet na Jean Francois Coupe waliowahi kuwa mawaziri katika serikali zilizotangulia za nchi hiyo pamoja na Jean Frederic Poisson mwakilishi katika Bunge la Ufaransa walishiriki katika mdahalo huo.