Dunia leo inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Wapestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20377-dunia_leo_inaadhimisha_siku_ya_kimataifa_ya_kushikamana_na_wapestina
Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu imelaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na kutangaza kuwa, kuendelezwa siasa za ukandamizaji za utawala huo kutaimarisha zaidi harakati zenye misimamo mikali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 28, 2016 23:31 UTC
  • Dunia leo inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Wapestina

Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu imelaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na kutangaza kuwa, kuendelezwa siasa za ukandamizaji za utawala huo kutaimarisha zaidi harakati zenye misimamo mikali.

Taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Watu wa Palestina imesisitiza kuwa, kuvamiwa ardhi ya Palestina na jinai zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina ndiyo sababu ya mgogoro wa muda mrefu zaidi duniani ambao umekuwa chanzo cha migogoro mingine si Mashariki ya Kati pekee, bali pia katika uga wa kimataifa. 

Wapalestina wanaendelea kuuawa huko Palestina

Taarifa ya jumuiya hiyo imesema, kuwalazimisha mamilioni ya raia wa Palestina kuwa wakimbizi, mauaji yanayofanywa kila siku na Wazayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina, mwenendo wa Israel wa kupuuza matakwa ya jamii ya kimataifa na kutotekeleza maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ndiyo kielelezo kikubwa zaidi cha dhulma na ukosefu wa usawa duniani. Jumuiya hiyo imezitaka nchi zote dunia kuchukua hatua za kimsingi za kutetea haki za Wapalestina.

Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiisalmu

Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu pia imeitaka jamii ya kimataifa hususan nchi za Waislamu kuchunguza kwa kina sababu za kuendelea mgogoro wa Palestina na njia za kuutatua ikiwa ni pamoja na kuitishwa uchaguzi huru utakaowashirikisha Wapalestina wote, Waislamu, Wakristo na Wayahudi, haki ya kujiamulia mambo yao na kuruhusiwa wakimbizi wote wa Palestina kurejea katika ardhi na nchi yao.

Mwaka 1977, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio lililoitambua tarehe 29 Novemba kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Wapalestina.