Ndege za kivita za Israel zaihujumu Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20467-ndege_za_kivita_za_israel_zaihujumu_syria
Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimevurumisha makombora manne katika maeneo mawili nchini Syria karibu na barabara inayounganisha mji mkuu wa Syria, Damascus na mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 30, 2016 04:22 UTC
  • Ndege za kivita za Israel zaihujumu Syria

Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimevurumisha makombora manne katika maeneo mawili nchini Syria karibu na barabara inayounganisha mji mkuu wa Syria, Damascus na mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Kwa mujibu wa tovuti ya Rai al Youm,  hujuma hiyo imetekelezwa leo Jumatano katika eneo lijulikanalo kama as Sabourah.

Taarifa zinasema kati ya eneo lililolengwa na makombora ya ndege hizo za utawala wa Kizayuni ni ghala la silaha na idadi kadhaa ya malori ya kijeshi yaliyokuwa yamebeba silaha na zana nyinginezo za kijeshi.

Tokea uanze mgogoro wa Syria zaidi ya miaka mitano iliyopita, jeshi la utawala haramu wa Israel, ambalo linawaunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Rais Bashar al Assad, limekuwa likitekeleza hujuma katika nchi hiyo ya Kiarabu hasa kwenye milima ya Golan ambayo inakaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.