Utawala wa Saudi Arabia wandelea kufanya mauaji ya kinyama nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i21733-utawala_wa_saudi_arabia_wandelea_kufanya_mauaji_ya_kinyama_nchini_yemen
Ndege za kijeshi za Saudi Arabia zimeendelea kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya raia huko nchini Yemen licha ya kuweko miito ya kuhitimishwa jinai hizo dhidi ya raia wasio na hatia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 19, 2016 11:13 UTC
  • Utawala wa Saudi Arabia wandelea kufanya mauaji ya kinyama nchini Yemen

Ndege za kijeshi za Saudi Arabia zimeendelea kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya raia huko nchini Yemen licha ya kuweko miito ya kuhitimishwa jinai hizo dhidi ya raia wasio na hatia.

Kanali ya Televisheni ya al-Masira ya Yemen imeripoti kwamba, leo mji wa Saidah umeshambuliwa zaidi ya mara 50 na ndege za kijeshi za Saudia na washirika wake.

Ripoti zinaeleza kwamba, mashambulio hayo ya leo ya ndege za kijeshi za Saudia  dhidi ya mji wa Saidah ulioko kaskazini mwa Yemen yamesababisha uharibifu mkubwa. Mtu mmoja anaripoti kuuawa katika hujuma hiyo ya ndege za kijeshi za Saudia huku makumi ya majengo yakibomolewa.

Aidha kiwanda cha saruji katika mkoa wa Taiz ulioko kusini magharibi mwa Yemen kimeshambuliwa na makombora ya ndege za kijeshi za utawala wa Aal Saud na washirika wake. 

Athari za hujuma ya kijeshi ya Saudia huko nchini Yemen

Wakati huo huo, jeshi la wananchi la Yemen limefanikiwa kukwamisha mashambulio ya mamluki wa Saudia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kuwaangamiza mamluki 12 na kuwajeruhi wengine wengi.

Majeshi ya Saudi Arabia na washirika wake kama Marekani, Israel na nchi kadhaa za Kiarabu, yalianza kulishambulia taifa la Yemen mwezi Machi mwaka jana kwa kisingizio cha kumrejesha madarakani rais aliyetoroka nchi na kukimbilia Saudia, Abd Rabbuh Mansur Hadi.  

Mashambulio hayo ya kinyama ya Saudia hadi sasa yameshaua zaidi ya Wayemeni elfu kumi, kujeruhi mamia ya maelfu ya wengine au kuwaacha bila ya makazi mbali na kuteketeza asilimia 80 ya taasisi za miundombinu na za utoaji huduma na tiba za nchi hiyo masikini ya Kiarabu.